Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT) Neema Msitha akizungumza na wanahabari kuhusu Tamasha la Michezo la Tanzanite litakalofanyika kuanzia Septemba 16-18 mwaka katika Viwanja vya Benjamin Mkapa.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Rais
Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la
Michezo kwa Wanawake 'Tamasha la Michezo la Tanzanite litakalofanyika
Viwanja vya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 16
hadi Septemba 18 mwaka huu.
Akizungumza na
wanahabari leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara
ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbas, Kaimu Katibu Mtendaji
wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya tamasha hilo Neema Msitha amesema siku ya kwanza ya
tamasha kutakuwa na kongamano la kujadil michezo na kwamba mada
mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu wabobezi.
“Hali halisi kuelekea kwenye tamasha letu iko vizuri, tunawakaribisha sana wanawake wote wa Dar es salaam na wamikoani pia mje mnufaike na mambo mazuri na mengi ya wanawake,’’amesema Msitha.
Amezitaja
baadhi ya mada hizo ni uhalisi wa wanawake katika kushiriki michezo,
maadili na taaluma ya michezo kwa wanawake pamoja na mchango wa vyombo
vya habari katika michezo.
Msitha amesemaTarehe 17 tamasha litapambwa na michezo nane ya wanawake kutoka katika timu vinara za taifa zikiwemo ngumi za wazi na kulipwa, Wanariadha kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, Mpira wa Netibali utakaoshindanisha timu ya JKT Mbweni na Uhamiaji, Mpira wa miguu kati ya timu ya Simba Queen na timu ya Taifa ya U 20, Mpira wa wavu kati ya timu ya Jeshi stars na Magereza, Mpira wa kikapu kati ya timu ya Don Bosco na JKT pamoja na timu ya watu wenye ulemavu kwa mpira wa kikapu.
Amesisitiza
kuwa vilabu vya michezo hiyo vimethibitisha kushiriki na kwamba siku ya
tatu ya mashindano hayo michezo itamaliziwa kwa washidi kupewa zawadi
na kwamba mgeni rasmi atakuwa Rais Samia.
Ameongeza
kuwa lengo ni kuendelea kumuunga mkono Rais Samia ambaye katika hotuba
zake ameonekana mafanikio ya timu za wanawake lakini hazitangazwi kama
za wanaume pamoja na kuhamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki
michezo kwani michezo ni ajira na hujenga afya.
No comments:
Post a Comment