RAYA HAMAD- OMKR
Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak amesema kwamba Zanzibar
imepiga hatua kubwa katika kupunguza virusi vinavyosababisha
maambukizi ya maradhi ya UKIMWI.
Dkt Shajak
ameeleza hayo leo alipozungunza na Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI Dkt Leopold Zekeng Ofisini kwake
Migombani mjini Zanzibar.
Amesema jitihada
zinazofanywa na serikali kupitia Tume ya inayoratibu mapambano dhidi ya
UKIMWI Zanzibar zimesaidia sana kuwepo mafanikio makubwa na kwamba
maambukizi yamepungua kutoka asilimia 0.6 hadi 0.4
Dk
shajak amefahamisha kwamba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea
na jitihada zake hizo ili kuwezesha kutimiza lengo la Zanzibar ifikapo
mwaka 2025 kusiwepo tena maambukizi mapya ya maradhi ya UKIMWI Zanzibar.
Aidha
alishukuru Shirika la Umoja wa Matafa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS)
kwa kuonesha nia ya kuendelea kuisaidia Tanzania katika harakati za
mapambano dhidi ya maradhi ya UKIMWI.
Amesema
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Tume ya UKIMWI inaendelea kutoa
elimu na kuhakikisha kuwa jamii inaongeza uelewa juu ya masuala mbali
mbali yanyohusu UKIMWI ili kuisaidia jamii kujiepusha na tabia
hatarishi zinazochangia kasi ya maambukuzi ya virusi vya maradhi ya
Ukimwi.
Nae Mkurugenzi mkaazi wa UNAID Dkt Leopold
Zekeng amesema Shirka hilo litaendelea kuisaidia Zanzibar kuunga mkono
jitihada za kupambana na UKIMWI ili kuhakikisha hakuna maambukizo
mapya kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto.
No comments:
Post a Comment