HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 27, 2021

KIJANA ADAIWA KUBAKA MBUZI

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia na kumuhoji kijana mmoja mkazi wa Rusaunga aliyetambulika kwa jina la Emmanuel Zakaria  mwenye umri wa miaka 38 kwa tuhuma za kufanya ngono na Mbuzi wa kike.


Taarifa ya tukio hilo imetolewa na kamanda wa polisi Mkoani Kagera Awadhi Juma wakati akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake.


Kamanda huyo amesema wakati mtuhumiwa huyo akiendelea na kitendo hicho alipita mke wa jirani yake na mlalamikaji na kumkuta  mtuhumiwa akifanya kitendo hicho hivyo kutoa taarifa kwa wananchi wengine kisha mtuhumiwa kuwekwa chini ya ulinzi.


Aidha kamanda amesema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na jeshi hilo amekiri kufanya tukio hilo huku akidai kuwa alizidiwa na tamaa za mwili ambapo kijana huyo anaendelea kuhojiwa katika kituo Cha polisi wilayani Biharamulo.

No comments:

Post a Comment

Pages