HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 27, 2021

JAJI MKUU PROF JUMA AENDELEA NA ZIARA YA KIKAZI MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 27 Oktoba 2021 ameendelea na ziara yake aliyoianza jana tarehe 26 Oktoba, 2021 Mahakama Kuu Kanda ya Musoma.

 Leo ametembelea Mahakama ya Mwanzo Robanda ambapo amepokea taarifa ya utendaji kazi wa Mahakama hiyo, ametembelea pia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti na baadaye amezungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti. Mhe. Prof.Juma ataendelea na ziara yake kesho katika Wilaya ya Tarime na Rorya ambapo pia atazungumza na Watumishi wa Mahakama hizo. Ziara hii itakamilika tarehe 29 Oktoba 2021.

 SIKU YA PILI YA ZIARA: Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni.

No comments:

Post a Comment

Pages