HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 28, 2021

MUSIBA KUMLIPA MEMBE FIDIA YA BILIONI 6

 


 

Na Mwandishi Wetu

MILIKI wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba leo amehukimiwa hukumu nyingine ya kumlipa fidia  Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Bernard Membe ya Sh.Bilioni 6 baada ya kuthibitishwa tuhuma za kumchafua kupitia vyombo vyake vya habari.


Hukumu hii imesomwa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakati ile ya awali ilisomwa mapema mwaka huu Mahakama Kuu Zanzibar ikimwamuru alimpe Fatuma Karume Sh. Billioni 7.5.

Hukumu hiyo  ni ya kesi namba 220/ 2018 na imetolewa na Jaji Joacquine De Mello ambapo amesema mbali na mambo mengine Musiba amlipe Sh. Bilioni 6 Membe, pia inatoa zuio la kudumu la kutomkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake na kulipa gharama za kesi.

Mahakama imesema Sh.Bilioni 5 ni fidia ya hasara halisi na Sh. Bilioni 1 hasara ya jumla, katika kesi hiyo Membe alimshtaki Musiba, Mhariri wa gazeti la Tanzanite na wachapishaji wa gazeti hilo ambapo aliwadai Sh. Bilioni 10 kwa kumchafua.

Musiba katika kesi hiyo alishtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.

No comments:

Post a Comment

Pages