HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 28, 2021

MAHAKAMA YAMUHUKUMU AVEVA KIFUNGO CHA MIEZI SITA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu  aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.

Hata hivyo, mahakama hiyo imemwachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa Klabu hiyo  Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu kutokana na ushahidi wa Jamhuri kushindwa kumtia hatiani dhidi ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

 Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba.

Alisema mahakama yake bila kuacha shaka upande wa Jamhuri umethibitisha mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya Aveva na kwamba mahakama yake inamtia hatiani.

"Mahakama yangu inamtia hatiani mshtakiwa wa kwanza Aveva dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka atakwenda jela kutumikia kifungo cha nje cha miezi sita" Alisema.


Akiichambua hukumu hiyo alisema hakuna ubishi kwamba  Dola za Kimarekani 300,000 ziliingizwa  kwenye akaunti ya Klabu ya Simba kupitia benki ya CRDB ambayo ni mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi.

Alisema baada ya kuingia kwenye  akaunti hiyo inaonyesha kwamba kamati tendaji ya  klabu ya simba ilielekeza itolewe fedha hiyo kwenye akaunti ya Simba ili itumike kwenye uwanja wa Bunju kujenga kwa nyasi bandia.

"Ushahidi umethibitisha kwamba Ile fedha ilitakiwa ijenge nyasi bandia kwenye uwanja wa Bunju lakini haikufanyika hivyo matokeo yake zilienda kwenye akaunti binafsi ya Aveva, kinyume cha maelekezo ya kamati hiyo"alisema Hakimu  Simba

Alisema  mahakama hiyo imejiridhisha kuwa mashtaka yote haijadhibitisha isipokuwa shtaka la matumizi mabaya ya ofisi ambayo ya kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Klabu ya Simba na kwenda akaunt binafsi.

Simba alisema kutokana na mashtaka hayo Nyange amekutwa hana hatia isipokuwa Aveva amekutwa na hatia Kwa kutumia nafasi yake vibaya kwa Kuingiza ongoza fedha hizo kwenye akaunti binafsi ingawa hakuna wizi uliofanyika.

"Hela zote zilitumika kihalali isipokuwa tatizo lake  hizo fedha ziliingizwa kwenye akaunti binafsi,alisema Simba.

Baada ya maelezo hayo Wakili wa serikali Fatima Waziri alidai hawana kumbukumbu ya makosa ya jinai yaliyotendwa na mshtakiwa huyo hivyo naiomba mahakama itoe adhabu Kali ili iwe funzo kwake na Kwa wengine wanaotumia madaraka vibaya ya ofisi.

Ndipo Wakilibwa utetezi Kuge Wabeya aliieleza mahakama hiyo kosa lake ninla Kwanza mshtakiwa ni mgonjwa amekutwa akihuthuria kliniki mara tatu Kwa wiki na ana familia inayomtegemea.

"Tunaomba itoe adhabu nafuu itakayowezesha kuhudhulia kliniki na wqkati akiwa anasubiliwa mshtakiwa alikaa mahabusu tangu mwaka 2017 Hadi mwaka 2020,"alidai Wabeya.

Hakimu Simba alisema kutokana na mazingira yaliopo ya kesi amezingatia hoja za pande zote mbili kuwa mtuhumiwa amekaa mahabusu Kwa muda mrefu mpaka pale mahakama ilipoona kosa la utakatulishaji haijadhibitisha.

"Kumpeleka gerezani Kwa maana kumfunga haitasaidia chochote kwani watakuwa wamemfunga mgonjwa ambaye utakuwa imesababisha usumbufu siyo Kwa mshtakiwa Bali hata magereza na jamii Kwa ujumla,"alisema Simba.

"Hata ukimpiga faini kubwa  bado haitasaidia chochote kwani asipolipa atalazimika kupelekwa gerezani hivyo adhabu pekee inayomfaa mahakama imeona atumikie kifungo cha nje miezi Sita na asifanye kosa lolote,"alisema

Simba alisema rufaa ipo wazi kwa yeyote hajaridhika na maamuzi hayo.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

Pages