Na John Marwa
TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' licha ya kupoteza bao 1-0 dhidi ya Benin jioni ya Leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, mchezo wa kundi J kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia Qatar 2020 bado matumaini yapo.
Kwa Matokeo ya Leo Stars anashuka hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi ikiwa ni mara baada ya timu zote kucheza michezo mitatu.
Benin walioibuka na ushidi dhidi ya Stars wamekaa kileleni wakifikisha pointi Saba huku Congo DR wakifikisha pointi tano kwa kuwafunga Madagascar mabao 2-0 huku Stars akisalia na pointi nne na Madagascar wakiendelea kubuluza mkia.
Ikiwa kila timu imesalia na michezo mitatu Stars bado inahitaji kutumia vema dakika 270 zilizoko mbele yao kwa kuanza na Benin hapo Oktoba 10 siku mbili zijazo.
Kisha Stars itakuwa na mchezo dhdi ya Madagascar kisha kumaliza na Congo DR.
Stars itahitaji kunfunga Benin na kufikisha pointi saba kisha Madagascar na kufikisha pointi 10 na mchezo wa mwisho wakihitaji kumfunga Congo DR hapa nyumbani bila kujali matokeo ya wapinzani wake moja kwa moja atakuwa na pointi 13 ambazo kiuhalisia zinaaweza zisifikiwa na Congo DR na Benin kama watakubali kupoteza kwa Stars na woa kwa wao kalizana.
Katika mchezo wa Leo Stars haijacheza vibaya lakini imekosa bahati kutokana na nafasi walizozitengeneza na kushindwa kuzitumia.
Kila la heri Taifa Stars Watanzania bado wanaimani na ninyi.
No comments:
Post a Comment