Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Ladislaus Mwamanga.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) umetengewa Sh Biloni 5.5
zitakazoelekezwa katika utoaji wa ruzuku na utekelezaji wa Miradi ya
Ajira za muda kwa kaya za walengwa ili zipate kipato cha kuziwezesha
kujikwamua kiuchumi na kupunguza athari za Uviko 19 pamoja na kuongeza
rasilimali na miundombinu ambayo itatumika na jamii yote katika Mitaa na
Shehia.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Ladislaus Mwamanga wakati
akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo
kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uvko 19 kwa Mpango wa kunusuru
Kaya za Walengwa wa TASAF.
Amesema kuwa fedha
hizo ziwafakikia kaya za walengwa 40,740 wenye uwezo wa kufanaya kazi
amabao wanaishi katika maeneo ya mjini, watafanya kazi za miradi ya
jamii na kulipwa ujira wa Sh 135,000 kwa kila kaya ili kufufua na
kuimarisha shughuli zao na kukuza uchumi wa kaya zilizoathirika zaidi na
ugonjwa huo.
" Mfuko umeidhinishiwa Sh Bilioni
5.5 kati ya fedha zilizotolewa kama mkopo wenye masharti nafuu kukoka
Shirika la Fedha Kimataifa (IMF) itazitumia fedha hizo kuondoa athari
za kiuchumi zilizochewa wa Uviko 19 kwa kaya walengwa ambazo Serikali
imedhamiria kuwaondoa katika umaskini wa kipato kwa kuwapatia ruzuku za
kujikimu, ajira za muda , kuwaongezea ujuzi, maarifa na elimu ya
ujasiriamali ili wakidhi mahiaji yao," amesema Mwamanga.
Amebanisha
kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mpango na mikakati mbalimbali
katika kupunguza umaskini wa watanzania wanaoishi katika mazingira duni
na kwamba inafanya jitihada kubwa kupata vyanzo vya ndani, mikopo na
misaada kutoka wadau wa maendeleo ili kuhakikisha watanzania
wanaondokana na umaskini.
Amesisitiza kuwa muda
wa matumizI wa fedha hizo umewekwa bayana na kwamba Menejimenti ya
TASAF kwa mwongozo wa Kamati ya Uongozi ya Taifa itahakkisha maandalizi
ya utekelezaji wa miradi ya ajira za muda kwa walengwa katika maeneo
yatakayoanishwa utaanza mara baada ya fedha hizo kupokelewa.
Amemshukuru
Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vyema mapambano dhidi ya UVIKO
19 ambayo yamefanikisha kupata mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za
Kimarekani Milioni 567 sawa na Sh Trilioni 1.3 kutoka IMF kwa ajili ya
Kampeni kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano ya Uviko huo.
Amemuhakikishia
Rais Samia kwamba utekelezaji wa miradi utafanywa kwa wakati na hakuna
fedha zitakazotumika nje ya malengo yaliyokusudiwa kwa walengwa wa
TASAF.
No comments:
Post a Comment