Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi rais wa TFF Wallace Karia wakionesha mkataba wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu wenye thamani ya shilingi bilioni 2.5 uliosainiwa leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi na Rais wa TFF Wallace Karia wakisaini Mkataba wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Bara wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.5.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Shirikisho
la Soka la Tanzania (TFF) limeitambulisha Benki ya Taifa ya Biashara
Nchini (NBC) kuwa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu wa
2021/22 kwa kutiliana saini mkataba wenye thamani ya Sh Bilioni 2.5.
Akizungumza
katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Rais wa TFF, Wallace Karia
amesema kwa sasa ligi hiyo itafahamika kwa jina la NBC Premier League
kwa kuwa benki hiyo ni wadhamini wakuu hivyo mchanganuo wa fedha
utatumika kwenye usafiri.
Amebainisha kuwa ligi
kuu imeanza kutimua vumbi pasipokuwa na mdhamini na kwamba kwa kipindi
cha miaka mitatu ligi hiyo itaitwa jina hilo huku akisisitiza kuwa ni
mwendelezo wa kuiboresha.
" Wakati wadhamini wa
kwanza wanaingia ligi kuu madhumuni makubwa ilikuwa kusaidia usafiri
wa kwenda na kurudi kwenye vituo vya mechi vya timu shiriki hakukuwa na
tatizo la timu kushindwa gharama za usafiri," amesema Karia.
Ameongeza
kuwa wa hawajabadili kitu kwani sehemu kubwa ya fedha hiyo itasaidia
vilabu kwenye suala la usafiri na kwamba sehemu ya mishahara
imeshashuhulikiwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi amesema wamefarijika kuingia udhamini kwa
kuwa mchezo wa mpira unafuatiliwa sana hapa nchini na kwamba kwa mujibu
wa CAF ligi kuu ipo nafasi ya 8.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi na Rais wa TFF Wallace Karia wakisaini Mkataba wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Bara wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.5(1).
No comments:
Post a Comment