HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 09, 2021

MAJALIWA: WATANZANIA WANAMATARAJIO MAKUBWA NA TAIFA STARS


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na Wachezaji baada ya mazoezi ya timu ya Taifa Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo utakaochezwa Alhamis Novemba 11, 2021.

 Wachezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa baada ya mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo utakaochezwa Alhamis Novemba 11, 2021.

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mazoezi ya timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars) na amewaeleza wachezaji kwamba Watanzania wanamatarajio makubwa kwamba timu yao itafuzu na kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika, Qatar 2022.

 

“Nimekuja kuona mwenendo wa mazoezi, matarajio tuliyonayo ni makubwa na tuna imani mtashinda. Mechi ya keshokutwa ni muhimu kwa nchi yetu tunahitaji kushinda mechi zilizobaki ili tutimize malengo yetu. Tunahitaji kuweka historia.”

 

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Novemba 9, 2021) wakati akizungumza na wachezaji wa Timu ya Soka ya Tanzania, (Taifa Stars) katika uwanja wa Benjamin William Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya kushuhudia mazoezi ya timu hiyo.

 

Taifa Stars inafanya mazoezi ya kuajiandaa na michezo ya awali ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Timu ya Taifa ya DR Congo na Madagascar, ambapo Mheshimiwa Majaliwa amewasisitiza wachezaji wazingatie mafunzo yanayotolewa na walimu.

 

Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia Wizara ya Michezo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wataendelea kuisimamia na kufuatilia maendeleo ya timu hiyo hadi hatua ya mwisho na kuhakikisha inafanya vizuri.

 

Kwa upande wake, Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye amezungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema wamejiandaa vizuri na kwamba watahakikisha wanapata ushindi katika mechi zote zilizobaki. “Tutapambana kwa ajili ya nchi yetu.”

 

No comments:

Post a Comment

Pages