HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 05, 2021

Rais Samia afanya ziara ya kustukiza kukagua ujenzi wa Daraja la Tanzanite


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatius Mativila kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Tanzanite linaloendelea kujengwa katika eneo la Selander Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo tarehe 04 Novemba 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Tanzanite linaloendelea kujengwa katika eneo la Selander Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo tarehe 04 Novemba 2021. Kulia ni  mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatius Mativila.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo tarehe 04 Novemba 2021. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo tarehe 04 Novemba 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo tarehe 04 Novemba 2021.

No comments:

Post a Comment

Pages