HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 17, 2021

TANESCO KYERWA YATAKIWA KUMALIZA MALALAMIKO KWA WANANCHI

Na Lydia Lugakila, Kyerwa

Baraza la madiwani wilayani Kyerwa mkoani Kagera limemtaka Meneja wa Tanesco kuhakikisha anatatua changamoto ya kukosekana kwa nishati hiyo pamoja na kukatika ovyo kwa umeme.

Hoja hiyo imeibuliwa  na diwani wa kata ya Iteera Devotha Biashara aliyetaka kujua shirika hilo limejipangaje kuondoa malalamiko toka kwa wananchi hasa vikundi vya akina mama wenye miradi ya maendeleo iliyohitaji kuendeshwa kwa nishati hiyo ikiwemo taasisi za kiserikali kukwama au kupigwa tarehe ya kufikishiwa huduma hiyo inapohitajika katika maeneo yao.

Akijibu hoja hiyo  Kaimu Meneja  wa Tanesco Wilaya ya Kyerwa, Godlisten Ayo, amesema kuwa malalamiko hayo yametokana na  ukosefu wa bajeti ambapo ameahidi kuyafanyia kazi kulingana na bajeti  itakavyoruhusu.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Kyerwa  Bahati  Henerco kupitia Baraza hilo ametoa mapendekezo na kumtaka Meneja Tanesco wilayani humo kuhakikisha anapunguza malalamiko hayo kufikia Januari  mwaka 2022.

"Hakikisha mnashughulikia matatizo yote, na kuondoa nguzo zilizolala chini kwa muda mrefu ili zipelekwe kuwahudumia wananchi na kuacha tabia ya kukaa ofsini"alisema Bahati Henerco.

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Rashid Mwaimu amemtaka  meneja huyo  kuhakikisha anafikisha umeme katika taasisi zote za umma, na maeneo ya wananchi ikwemo shule ya Nyamilima, Rutunguru ambazo hazina huduma hiyo huku akitaka kupata taarifa ya utekelezaji wa maagizo hayo.

"Nahimiza Tanesco hakikisha sehemu zote zenye Transfoma ikiwemo Nyakatete suala hilo lifanyiwe kazi, maliza changamoto zote ili wananchi watekeleze miradi yao bila usumbufu.

No comments:

Post a Comment

Pages