HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 07, 2021

Wajasiriamali watakiwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kukuza masoko yao


Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa akisisitiza jambo kwa wajasirimali katika tamasha lililoandaliwa na serikali ya mtaa wa Bonyokwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Vijana Light of Success.

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

 

KATIBU Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa amesema matumizi ya teknolojia ni muhimu kwa wajasiriamali ili kukuza  masoko ya bidhaa zao pamoja na kujifunza kupitia watu wengine.

Pia amewataka wajasiriamali wawe na bidii, kutambua fursa, kuwa na malengo kuhakikisha biashara zao hazibaki kama ilivyo sasa na badala ya wapige hatua.

Hayo amesema jana jijini Dar es Salaam wakati akifunga tamasha siku moja la  wafanyabiashara na wajasiriamali lililoandaliwa na serikali ya mtaa wa Bonyokwa iliyopo wilayani Ilalla kwa kushirikiana na Taasisi ya Vijana Light of Success.

Amesema wao kama baraza la ni taasisi inayosimamia sera ya uwekezaji  mambo ambayo  wanasisitiza ni wajasiriamali kuwa na majuukwaa ya kuwakutanisha.

" Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza majukwaaa haya yaendelee kwa kuwa yanawasaidia wajasiriamali kujenga uwezo, kimtaji, kiuchumi,kimasoko na kufungua fursa kwa ajili ya wajasiriamali, " ameongeza.

Nasisitiza hili  kama baraza la uwezeshaji  naona kama njia ambayo anaweza kujikwambua mjasiriamali," amesema Katibu huyo Mtendaji.

Ameongeza kuwa majukwaa yanasaidia kukutana na Taasisi za uwezeshaji ambazo zinasaidia kuboresha biashara na kwamba hilo ni tamasha la kujifunza vitu mbalimbali kama wajasiriamali wafahamu mambo ya kuzingatia pia fursa za serikali.

Amesema kupitia tamasha hilo amejifunza mambo mazuri yanayofanyika katika Kata ya Bonyokwa ikiwamo kuona kiwanda cha kuchakata uchafu ambacho kinatengeneza mbolea na wadudu kwa ajili ya mifugo.

"Kiwanda hiki hakina harufu ni kisafi unaweza kukaa na kula chakula, hii ni teknolojia nzuri na ubunifu wa hali ya juu na watu wengine waweze kujifunza kupitia kata hii," amesema.

Naye mfanyabiashara wa kutoa huduma za kijamii
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya  Harmony Memorial Poltclinic Jullyan Mmary amesema wanaokatisha tamaa ni wenye taalama kwa kusema kuwa huwezi kufungua hospitali, kituo cha afya kama sio daktari.

Mkurugenzi huyo ambaye pia ni mwezeshaji wa tamasha hilo  amesema serikali kupitia wizara zake  ngazi zote kuanzia chini hadi juu kila kitu kipo wazi kwa mtu yoyote anaye kwenda anaelekezwa  utaratibu kwa upendo mkubwa.

" Ninachoweza kuwaambia wajasiriamali wajitambue, kuthamini mawazo yao na kuamini katika kitu wanachokifanya watafanikiwa na kufikia hatua ya kuwa wafanyabiashara," amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Bonyokwa Shabani Maliyatabu amewataka vijana, akina mama, baba na watu wenye ulemavu waendelee kuunda vikundi vya kijamii na vya kiuchumi kwani fursa za kimaendeleo zipo.

Amesema serikali imeiamini Bonyokwa  na kuwapatia vijana waliopo kwenye kikundi kiasi cha fedha Ml. 210 kwa ajili ya kujikwambua kiuchumi.

" Fedha hizi ni zile asilimia 10 zinazotolewa na Halmashauri katika mgawanyo wa makundi matatu asilimia 4 kwa akina mama, 4 nyingine kwa vijana na 2 kwa watu wenye ulemavu, " anesema Maliyatabu.

Ameongeza kuwa vijana hao tayari wameajiri vijana wenzao  baada ya kununua daladala mbili, gari ya kubeba mizigo  1 na kufungua kiwanda cha kufyetua  matofali na kwamba hiyo imefungua fursa kwa vijana wengine.

No comments:

Post a Comment

Pages