Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata zaidi ya watu 26
wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo matukio ya kuvunja na
kuiba vitu vya watu pamoja na biashara ya dawa za kulevya aina ya Bangi.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Kanda
hiyo Jumanne Muliro (pichani) ambapo amesema watu hao wamekamatwa katika
oparesheni kali iliyofanyika kwa wiki mbili na kwamba watuhumiwa
wamekutwa na Kompyuta mpakato zaidi ya (9), Gari la wizi moja aina ya
Toyota Wish No. T 189 DBZ na Runinga 15.
"
Jeshi la Polisi la Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika oparesheni kali
zinazolenga kuwakamata wahalifu limewakamata zaidi ya watu ya 26
wanaojihusisha vitendo vya uvunjaji na kuiba mali hii yote imefanyika
wiki mbili ya oparesheni kali, " amesema Kamanda Muliro.
Amebainisha
kuwa katika operesheni hiyo watu wanaofanya biashara ya Bangi wakitumia
Bajaj kusafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine pamoja na gari
linalotumika kubeba mali za wizi zilizokamatwa.
Amesisitiza
kuwa watu wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani kwa ajil ya
kuchukuliwa hatua za kisheria huku akikazia jeshi hilo halitafumbia
macho vitendo vya uhalifu.
Katika hatua
nyingine, jeshi hilo limetoa tahadhari na onyo kuelekea Sherehe za Miaka
60 ya Uhuru wa Tanzania kwa watu wanaopanga njama au kushiriki kufanya
vitendo vya uhalifu litawashughulikia zaidi ya sheria.
Pia
Kamanda Muliro amewashukuru wananchi wanaoshirikiana na polisi kutoa
taarifa zinazofanikisha kuwakamata wahalifu na kuwaomba waendelee
kufanya hivyo kukomesha vitendo vya uhalifu.
No comments:
Post a Comment