Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akikabidhiwa Viti na Meza 100 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magese kwa ajili ya Chuo cha Afya Mpanda,Viti hivyo ni msaada kutoka Benki ya NMB Kanda ya Magharibi.
Na Mwandishi Wetu, Mpanda
Benki
ya NMB imekabidhi msaada wa viti na meza 100 zenye thamani ya sh. Mil
10 kwa chuo cha afya Mpanda mkoani Katavi katika kusaidia uboreshaji wa
miundombinu kwenye sekta ya Elimu na Afya kwa hapa nchini.
Makabidhiano
hayo yalioongozwa na Meneja wa benki ya NMB kanda ya Magharibi,
Sospeter Magese na kushuhudiwa na mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua
Mrindoko yalifanyika chuoni hapo Mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Bw. Sospeter alisema kuwa imekuwa desturi
ya benki ya NMB kutenga asilimia moja ya faida yake baada ya kodi kwa
ajili ya kusaidia jamii inayowazunguka kwani jamii hizo ndio zimeifanya
benki ya NMB kuwa benki kinara hapa nchini.
“kwa
zaidi ya miaka saba sasa tumekuwa tukitenga asilimia moja ya faida ya
benki kwaajili ya kusaidia jamii zetu katika nyanja za elimu, afya na
kunapotokea majanga mbalimbali. Kuzisaidia jamii zetu imekuwa desturi
yetu kwani jamii hizi ndizo zimekuwa chachu kubwa ya sisi kama benki ya
NMB kufanya vyema na kufika hapa tulipo,” alisema.
Mbali
na misaada kwa jamii, Meneja huyo alisisitiza juu ya mikopo rafiki
inayotolewa na benki ya NMB katika sekta ya kilimo na ufugaji huku
akasisitiza juu ya kuchukua mikopo hii kwani ndio chachu ya maendeleo ya
uchumi.
Aidha,
Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko aliipongeza benki ya NMB kwa
moyo wao wakujitoa na kusaidia jamii zao huku akiwashukuru kwa msaada
walioutoa kwa chuo cha afya Mpanda na kuisihi benki ya NMB kutochoka
kusaidia jamii na hususani mkoa wa Katavi.
Bi
Mrindoko alisema, “Binafsi niwapongeze sana kwa kujitoa kwenu kwani
mmekuwa ni chachu ya maendeleo kwa mkoa wetu, tunazidi kuwashukuru sana
na kuwaomba msichoke kuzisaidia jamii za Kitanzania na ikiwapendeza
mzidi kuleta misaada katika sekta hizi za Afya na elimu kwa mkoa wetu wa
Katavi.”
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Lightness Michael aliiomba benki ya NMB
kuendelea kutoa misaada kwa chuo hicho kwani bado wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali zikiwemo uchache wa madarsa ambao kama utatatuliwa
basi wataongeza udahili wa wanafunzi katika chuo hicho.




No comments:
Post a Comment