Vibarua wanaojenga kianda hicho a Tanzania na Burundi, akimsikiliza Waziri Mkuu alipokuwa akizungumza.
Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde, akitoa salamu za wakazi wa jimbo lake.
Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameridhishwa na Maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha kutengeneza mbolea (Intracom) kilichopo Nala jijini Dodoma chenye uwezo wa kuzalisha tani 600,000 za mbolea.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo mara baada ya kukagua ujenzi wa Kiwanda hicho ambapo amesema kufuatia uwepo wa Kiwanda hicho nchi itakuwa na upungufu wa mbolea laki moja huku akiwaagiza wataalam kilimo kukisaidia Kiwanda cha Minjingu kuzalisha mbolea inayokidhi mahitaji ya udongo wa hapa nchini ili kutosheleza mahitaji ya tani700,000 zinazohitajika nchini.
Aidha Waziri Mkuu amemuhakikishia mwekezaji ulinzi na usalama na kwamba Serikali ipo naye na itamsaidia kwa chochote huku akimtaka kwenda ofisi yoyote na kueleza changamoto itakayojitokeza ili ipatiwe ufumbuzi mapema huku akimuagiza Mkuu wa mkoa wa Dodoma kuhakikisha huduma katika eneo la Kiwanda zinaboreshwa ikiwemo kujenga barabara inayopitika muda wote lakini pia kuhakikisha huduma ya maji inaboreka.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kukamilika kwa Kiwanda hicho kutasaidia kuokoa Dola milioni 450 ambazo hutumika kila mwaka kuagiza mbolea nje ya nchi.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amemuhakikishia mwekezaji kwamba usalama upo na wa kutosha huku akisema wizara yake pia itakaa kupitia sheria ambazo zimekuwa vikwazo kwa wawekezaji kutoka nje ili kuviondoa.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Exaud Kigahe amesema watahakikisha wanaweka mazingira wezeshi ya Uwekezaji kwa wawekezaji toka nje ili kuweza kuwekeza hapa nchini.
Awali Akizungumza kwa niaba ya Mmiliki wa Kiwanda hicho Cha Mbolea,Msemaji wa Kiwanda hicho Nduwimana Nazaire amesema kuwa kukamilika kwa Kiwanda hicho kitasaidia kutoa Ajira 3000 kwa wananchi na kuahidi kukamilisha ujenzi wa Kiwanda Mwezi Mei Mwaka huu na kumshukuru Rais kwakuwakubalia kuwekeza Tanzania.
No comments:
Post a Comment