HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 02, 2022

BEN'S AGRO STAR YASHUSHA TANI 70 ZA VIUATILIFU VYA ZAO LA PAMBA

 


Sehemu ya shehena ya Viuatilifu aina ya Ben's Attack vilivyoagizwa na Kampuni ya Ben's Agrostar kupitia ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka India kuja Dar es Salaam vikiingizwa kwenye kontena tayari kwa kusafirishwa kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya wakulima wa zao la Pamba.

Mkurugenzi wa Masoko na Biashara wa Kampuni ya Ben's Agrostar ya Dar es Salaam, Patrick Mwalunenge, akizungumza na waandishi habari mara baada ya kupokea shehena ya Viuatilifu vya zao la Pamba. 


NA MWANDISHI WETU

WAKULIMA wa zao la Pamba wa Kanda ya Ziwa na mikoa jirani, wamehakikishiwa upatikanaji wa haraka na nafuu wa Viuatilifu kuelekea msimu wa kilimo cha zao hilo, ambalo ni miongoni mwa mazao ya kimkakati yanayopewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Sita.

Msimu wa kilimo cha Pamba umekuwa ukiandamwa na uhaba na ughali wa pembejeo, vikiwamo Viuatilifu muhimu kwa usatwi wa zao hilo na kudumaza mavuno ya wakulima, changamoto ambayo msimu huu imepata majawabu ya haraka kupitia uagizwaji na uingizwaji kwa njia ya ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), badala ya meli ambazo huchukua muda mrefu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Masoko na Biashara wa Kampuni ya Ben's Agro Star, Patrick Mwalunenge, wakati akipokea tani 12 kati ya 70 za Viuatilifu aina ya Ben's Attack, vinavyosafirishwa kwa haraka kupitia ATCL, kutoka India kuja Tanzania, safari inayochukua takribani saa 8, tofauti na meli ambazo zingesafirisha mzigo huo kwa siku 30 majini.

Mwalunenge alisema kuwa, ATCL inayofanya safari zake mara mbili kwa wiki kuja Tanzania, itatumika kusafrisha tani zingine 58 na kukamilisha tani 70, lengo la aina hiyo ya usafirishaji ukiwa ni kuwahi mahitaji ya wakulima katika msimu huu wa kilimo na kwamba gharama nafuu zinazotumika, unawapa wakulima hao uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei.

"Uagizaji huu una lengo la kuwahi msimu, lakini pia gharama nafuu za usafirishaji unaakisi unafuu wa bei tutayouzia bidhaa hii ambayo inaenda kusaidia kuwapa wakulima sababu ya kumudu manunuzi na kupuliza mashambani ili kuongeza ubora na uwingi wa mazao na kukuza pago lao na la Taifa kwa ujumla.

"Wito wangu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali nchini ni kutumia huduma za ATCL ili kuharakisha uingizwaji wa bidhaa wanazoagiza, lakini pia kusapoti harakati za Serikali katika kuiendesha Kampuni hiyo ya kizlendo," alisema Mwalunenge.

Aidha, Mwalunenge aliishukuru Wizara ya kilimo na Bodi ya Pamba Tanzania kwa sapoti yao katika kufanikisha uagizwaji na uingizwaji Viuatilifu hivyo, ambavyo vinaenda kuwahakikishia wakulima utatuzi wa changamoto za uhaba na ughali wa pembejeo hizo muhimu.

No comments:

Post a Comment

Pages