NA HAMIDA RAMADHAN, DODOMA
MKUU Wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesimamisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa mkoani hapa ili kuruhusu timu ya wataalamu kutoka mkoa kufanya uhakiki wa vifaa vya ujenzi vilivyonunuliwa na kiasi fedha kilichobaki.
Agizo hilo limekuja baada ya hospitali hiyo kujengwa kwa kusuasua na kushindwa kumalizika tangu ilivyoanza mwaka 2020 licha ya serikali kutoa fedha sh.bilion 1.8
Akizungumza Wilayani Kondoa mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa hospitali hiyo Mtaka alisema inasikitisha kuona serikali inatoa fedha kwaajili ya kuboresha huduma kwa wananchi lakini wanatokea watu wachache wanakwamisha jitihada hizo.
“ Sasa nasema kwamba shughuli zote za ujenzi zisimame ili siku ya jumanne Mhandisi wa Mkoa Happy Mgalula na Aziza Mumba watakuja hapa ili kuhakiki vifaa vya ujenzi vilivyonunuliwa na kiasi cha fedha kilicho baki katika akaunti ya benki,”amesema
Ameongeza kuwa:”Hakuna kitakacho haribika nikisema nasimamisha kazi za ujenzi kwasababu wamezoea siku zote hawapo kwenye eneo la ujenzi kwahiyo kama kuna zege limalizike leo baada ya hapa mkuu wa wilaya mkahakikishe vitu vyote vina baki stoo ili kusubili siku ya kuhakiki,”alisema
Mtaka amesema baada ya uhakiki wataalamu kutoka mkoa kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya wilaya watasimamia ujenzi wa hospitali hiyo hadi pale itakapokamilika.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk Khamis Mkanachi amekili kuwepo kwa changamoto ya kutokuelewana kati ya wanaotekeleza mradi na viongozi wa ngazi ya kata hadi wilaya
Amesema wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali na zitapotatuliwa wanakuja na kitu kingine na kumuomba mkuu wa mkoa atoe maelekezo na wao wapo tayari kuyatekeleza
“Nikweli kulikuwa na changamoto za hapa na pale lakini tulijitahidi kadri ya uwezo wetu kuhakikisha tunatatua lakini mradi huu umekuwa ukienda kwa kususua wakati mwingine tukifika hapa hatukuti mafundi kabisa lakini ukiuliza maneno yanakuwa mengi,”amesema
Dkt Mkanachi amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuleta wataalamu na kumhakikishia kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha ili mradi ukamilike na wananchi wapate hudima kama ilivyo adhma ya serikali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa wilaya ya kondoa wamesema hospitali hiyo imeanza kujengwa kwa muda mrefu lakini haikamiliki.
Mkazi wa Haubi Mariam Said amesema Hospitali hiyo iliwekwa jiwe la msingi tangu mwaka juzi lakini hadi sasa hawaelewi kwanini imeshindwa kukamilika licha ya kupewa taarifa kuwa serikali ilishatoa fedha.
Amsema wanapata shida hasa pale mtu napo pata rufaa ya kupelekwa katika hopitali ya mkoa gharama zinakuwa nyingi ikilinganisha na kama hospitali ingekuwepo hapo wilayani.
“Tunaomba serikali iingilie kati hospitali ikamilike Kwani tunapata changamoto hasa sisi wakina mama, ujenzi umeanza muda mrefu wakati mwingine tukipita pale hatuoni kabisa mafundi, wengine tulishajenga nyumba zetu zikakamilika lakini hospitali hadi leo iko palepale,”amesema
No comments:
Post a Comment