HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2022

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam lamshikilia mwanaume kwa kumpiga mtoto, lawashikilia 12 kwa wizi mitandaoni

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.
 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia mwanaume mmoja Mkazi wa Chamanzi Jijini Dar es Salaam kwa kosa ya kumpiga hadi kuzimia mtoto wake wa darasa la 3 kwa madai ya kuiba Sh 195000/= pamoja na watuhumiwa 12 kwa kosa la kujihusisha na wizi kwa njia ya mitandao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Kanda hiyo, ACP Jumanne Muliro amesema oparesheni iliyofanyika waliwakamata watuhumiwa hao na Kompyuta Mpakato moja mali ya kampuni ya tigo , Mashine ya Kielektroniki (EFD) ,simu za mkononi 42, kadi za tigo (line) 56 nyaraka zenye kurasa 1500 ambazo ni taarifa za mawakala wa mtandao wa tigo nchi nzima zenye taarifa za wateja wa Benki ya CRDB ambapo vielelezo vyote hivyo walikuwa wakitumia kufanya wizi.

Katika tukio lingine jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa mmoja Haji Mussa (30) kwa kosa la kumpiga mtoto wake wa kambo Feisal Masawe (11) mchaga mwanafunzi wa darasa la tatu anayesoma Shule ya Msingi Chamazi Dovya kwa fimbo na kumsababishia maumivu makali hadi kuzimia akimtuhumu kumuibia Sh 195,000/.

Kamanda amebainisha kuwa, Februari 23 mwaka huu mtoto huyo alifika shuleni na ilipofika saa sita na nusu aliondoka ili kurudi nyumbani akiwa njiani alidondoka njiani na kupoteza fahamu wasamaria wema walimuokota na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) ambapo alipatiwa matibabu na uchunguzi ulipofanyika ulionesha mtoto alikuwa amepigwa kipigo kilichomzidi.

No comments:

Post a Comment

Pages