HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2022

BUWEA YAHIMIZA WANACHAMA WAKE KUREJESHA MIKOPO KWA WAKATI

 


Consolattha Emmanuel akizungumza na wanachama katika mkutano mkuu.
Sehemu ya wanachama wa Buwea Saccos.

Na Lydia Lugakila, Bukoba


Chama cha Bukoba Women Empowerment Association (BUWEA) Manispaa ya Bukoba  mkoani Kagera kimetoa siku 4 kwa wanachama wake walioshindwa kurejesha  mikopo na riba kwa wakati kuhakikisha wanalipa mikopo hiyo kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Kauli hiyo imetolewa na Bi Consolatha Emmanuel ambaye ni msimamizi wa mikopo manispaa ya Bukoba katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa chuo Cha Carumco halmashauri ya wilaya ya Bukoba.

Bi Consolatha amesema kuwa kikundi hicho ni kwa ajili ya kuwakwamua wanawake kiuchumi, lakini malengo hayo yanakwenda kinyume na matarajio yao kutokana na baadhi ya wanachama kukwamisha maendeleo kutokana na kushindwa kulipa mikopo na riba kwa wakati jambo ambalo amelitaja kumnyima usingizi.

" Tangu mwezi Agosti 2020/ 2021 mwanachama anasema nitarejesha tumevumilia sana tumechoka, sasa ni mwezi Februari hakuna kinachoendelea sasa basi ifikapo Marchi Mosi mwaka huu sheria inaanza kufanya kazi" alisema Consolatha.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kikundi hicho Bi Rachael Ndyamukama amesema kuwa hafurahishwi na mienendo ya baadhi ya wanachama hao na kwamba wanatakiwa kujua taratibu za Saccos zilivyo hivyo wale watakaokiuka mikakati iliyowekwa katika ukopaji na urejeshaji wa mikopo hatua zichukuliwe dhidi yao kwani wanachangia kudidimiza kikundi.

Aidha kwa upande wake Polina Beda ambaye ni Katibu wa BUWEA amesema atahakikisha anafuatilia wale wote ambao ni wadaiwa sugu, wasiorejesha mikopo na riba kwa wakati.

Nao baadhi ya wanachama wa kikundi hicho akiwemo Bi Odetha Alexander na Vedastina Rambart wamekili kuwepo kwa hali hiyo na kuwashauri wenzao kuhakikisha wanafanya kila liwezekanalo ili kuwezesha wanachama wengine kukopa zaidi.

Hata hivyo Buwea Saccos ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa na jumla ya wanachama 457 ambapo Kati ya hao walio hai ni 447 wasio hai ni 6 na waliofariki ni  4.

No comments:

Post a Comment

Pages