HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 23, 2022

LHRC: KUNA HAJA YA KUWA NA CHOMBO HURU CHA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA JESHI LA POLISI

Na Asha Mwakyonde, Dodoma


KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kuna haja ya kuwa na chombo huru cha kuchunguza tuhuma dhidi ya Jeshi la Polisi nchini au vyombo vya usalama.


Haya yamesemwa jana jijini Dodoma na Afisa Uchechemuzi kutoka LHRC,William Maduhu katika semina ya baadhi ya wabunge vinara wa kupinga ukatili wakati akiwasilisha Wasilisho fupi juu ya uhitaji wa kuwa na chombo huru cha kushughulikia malalaniko yatokanayo na mauaji ya wananchi wangali vituo vya polisi na vitendo vingine vya kimaadili na utovu wa nidhamu wa baadhi ya polisi hao wasio waaminifu.


Afisa huyo amesema LHRC kama mdau katika masuala ya Utawala Bora na Haki za Binadamu wanapendekeza majina 13 ya chombo hicho kuwa ni Tume ya kushughulika na vitendo vya utovu wa nidhamu na mauaji ya wananchi wakiwa chini ya ulinzi( An independent Police Oversight Civilian Body), kuwe na Mwenyekiti wa chombo hicho ambaye atakuwa jaji Mstaafu wa Mahakama kuu au Mahakama ya Rufani atateuliwa na Rais.


Maduhu ameongeza kwamba kuwe na Katibu Mkuu ambaye atateuliwa na Rais, kuwe na wajumbe 10 kutoka katika taasisi za Mahakama,Ofisi ya Mkurugenzi vwa Mashtaka (DPP),Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Umma na Utawala Bora, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Tume ya Utumishi ya Wizara ya Mambo ya Ndani na kwamba wajumbe hao watateuliwa kutoka pande zote Tanzania Bara na Zanzibar. 


Maduhu ameeleza chombo hicho mbali na kuchunguza, kushughulikia malalamiko hayo kitaongeza heshima ya jeshi la polisi na kuonesha kuwa serikali inahakikisha wananchi wanapata haki zao kwa kuwa na mifumo thabiti yenye kuaminika katika jamii.


Amesema pamoja na kuwapo kwa mfumo wa utatuzi wa migogoro na ushughulikiaji wa malalamiko ndani ya jeshi hilo au vyombo vya usalama, bado kuna haja ya kuwa na mfumo wa nje utakaoshughulikia malalamiko hayo ya matumizi makubwa ya nguvu, utovu mkubwa wa nidhamu.


Maduhu amefafanua kuwa vitendo vya utovu wa nidhamu ni kama vitendo vya rushwa, kujichukulia sheria mkononi ndani ya jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama. 


"Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba jeshi la polisi haliwezi kuwa mtuhumiwa na likajuchunguza lenyewe.Hii inaashiria jeshi kama taasisi ya Umma linahutaji kuwa na chombo huru cha kushughulikia malalamiko ya wananchi ikiwamo mauaji wangali mikononi mwao," amesema.


Ameongeza kuwa chombo hicho kitakuwa huru hakitaingiliwa na mamalaka yoyote wakati kinatekeleza majukumu yake  na kwamba kitaongeza nguvu na ufanisi wa mfumo uliopo sasa ndani ya jeshi hilo kwa kusaidia mfumo huo.


Naye mbunge wa Mlalo Lushoto Tanga, Rashid Shangazi amesem kuwa kuna changamoto mbalimbali za ukuaji wa teknolojia na utandawazi hivyo kuna haja ya kuangalia muundo mzima wa jeshi la polisi na ikiwezekana kuwa na idara ambayo itahusika na uchunguzi pamoja na upelelezi.


" Wenzetu hawa  wa LHRC, waneona hili  na leo (Jana),wakatuchokoza mada kwa wabunge vinara wa kupinga ukatili," amesema Shangazi.


Kwa upande wake mbunge wa Viti  Maalumu wa chama Cha Mapindizi (CCM), Neema Lugangira ameiomba  tume hiyo pamoja na chama Waandishi wa Habari Kusini mwa Afrika (MISA- TAN), kushirikiana na wabunge hao  vinara wa kupinga ukatili wa kijinsia  kwa wanawake wanasiasa.


Amesema hajawahi kusikia sauti ya LHRC katika agenda ya kupinga ukatili kijinsia mitandaoni kwa wanawake wanasiasa.


"Tumepata semina kupitia Tume hii ushauri ninaoutoa ni tunapochagiza  masuala ya sheria na haki za binadamu ni vema kituo hiki kikabeba agenda ya ukatili wa kijinsia ya mitandaoni kwa wanawake wanasiasa," amesema.


Ameongeza kuwa kati ya vitu vikubwa ambavyo wanataka kufanya katika kuimarisha haki ni pamoja na ukatili wa kijinsia ambao ni mkubwa unasababisha kufifisha na kudumaza ushiriki wa wanawake wanasiasa mitandaoni.


Mbunge huyo ameeleza kuwa wanapitia ukatili mkubwa ambao ni mahususi kwa kuwa ni wanawake huku akitolea mfano mbunge mwanamke anawasilisha hoja yake mtandaoni aliyoiwasilisha bungeni.


Amefafanua kuwa hoja hiyo haitajadiliwa katika muktadha wa hoja husika bali itabadilishwa na kuanza kunadiliwa katika jinsia ya kike na kudai kuwa jambo ambalo ni hatari na linasababisha wanawake wengi wanasiasa kutoshiriki mtandaoni.


Mbunge huyo amesema kuwa hali hiyo inawanyima  haki ya kutumia mitandao na kuleta changamoto kubwa na hata wanawake na mabinti ambao wanatamani kuingia kwenye siasa wanarudi nyuma baada ya kuona wenzao wanavyofanyiwa.

No comments:

Post a Comment

Pages