HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 23, 2022

MHANDISI KUNDO: JESHI LA POLISI TOENI MAFUNZO KWA NJIA YA VITENDO NA NADHARIA KATIKA DUNIA YA UTANDAWAZI

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Mathew Kundo akizungumza wakati akifungua mfunzo ya siku tano ya makosa ya kimtandao kwa wapelelezi na Askari wa chumba cha Mashtaka.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma


NAIBU Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Mathew Kundo amelitaka Jeshi la Polisi Nchini kuhakikisha wanatoa mafunzo kwa Vijana wao kwa vitendo na nadharia kwenye dunia ya sasa inayokumbana na vita ya kimtandao hususani wahalifu wa mtandaoni.


Mhandisi Kundo ameyaeleza hayo jana Jijini Dodoma wakati akifungua mfunzo ya siku tano ya makosa ya kimtandao kwa wapelelezi na Askari wa chumba cha Mashtaka.


Ameibainisha kuwa ni lazima wahakikishe jeshi la Polisi na wataalamu wake wanakuwa wa kisasa na wanakwenda kujibu haja na kiu ya wanatanzania katika suala zima la makosa ya kimtandao mana wataweza kutoa elimu kwa kina.


Awali akizungumza kwaniaba ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DCI),Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Deusdedit Nsimeki,amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuwa na uelewa mpana wa sheria ya makosa ya mtandao na kuifanya taaluma hiyo katika kumsaidia mwananchi wala sio kujipatia kipato kutokana na kuwepo kwa  malalamiko toka kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa na kesi ya kupotelewa na simu zao kulipia gharama kubwa tofauti na simu ambayo imepotea na hivyo kuharibu taswira ya jeshi na taaluma kwa ujumla.


Naye Kamishna wa polisi uchunguzi wa kisayansi (CP),Shabani Hiki,amesema wao kama ma cro ni kama msingi katika nyumba kwani taswira ya Jeshi la polisi ipo kwao hivyo jukumu lao ni kufanya kazi kwa bidiii na kwa uadilifu mkubwa kwa kupunguza malalamiko.

No comments:

Post a Comment

Pages