HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 02, 2022

Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu


Na Asha Mwakyonde, Dodoma


Aliyekuwa Mtayarishari wa vipindi na Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Zuhura Yunus Abdallah (pichani) ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Katika taarifa iliyotolewa  jijini Dodoma leo na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Jaffar Haniu ilisema kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Zuhura kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Pia taarifa hiyo imesema kuwa Zuhura amechukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Haniu.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa uteunzi huo umeanza Januari 30, mwaka huu na kwamba Haniu atapangiwa kazi nyingine.

No comments:

Post a Comment

Pages