HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 25, 2022

Wakazi Mbagala kuanza kutumia mabasi yaendayo haraka Machi 2023

Mtendaji Mkuu wa wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) Dkt. Edwin Mhede, akizungumza na waandishi wa habari. 

Msimamizi wa Kitengo cha Kaizen kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Jane Lyatuu. 


 Na Julieth Mkireri


WAKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salam wanatarajia kuondokana na kero ya usafiri ifikapo Machi 2023 utakapoanza usafiri wa mabasi ya mwendo kasi.


Akizungumza na waandishi waandishi wa habari mjini Kibaha Mtendaji Mkuu wa wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) Dkt. Edwin Mhede alisema kwasasa mradi wa ujenzi umefikia asilimia 44.4.


Dkt Mhede alisema kwa mujibu wa mkataba wa Mkandarasi mradi huo utakamilika mwishoni mwa mwezi Machi 2023 na  wanapopokea barabara DARTwatakauwa wanakabidhi mtoa huduma wa mabasi yaendayo haraka.


"Licha ya mafanikio na vikwazo ambavyo vilikuwa vinaonekana kwenye sekta yetu ya usafirishaji Wizara ya Viwanda na biashara chini na Taasisi  ya CBE, SIDO na kitengo chake cha  Kaizen imeona itushirikishe DART ione iliyofanya kwenye viwanda kama yanaweza kuleta tija na kwenye sekta yetu.


Katika mafunzo ambayo tumeyapata tunahitaji kuwa na mabadiliko ya kifikra baina yetu DART na UDART tumekubaliana kufanya maboresho kwenye huduma zetu kuondoa karaha kwa wateja wetu wakiwemo wa ruti za Kibaha na maeneo mengine" alisema.


Mtendaji mkuu huyo alieleza kuwa wanatarajia kuondoa vikwazo kwa wakazi wa Kibaha kwenye uhitaji wa gari za moja kwa moja kutoka Kibaha hadi Kariakoo.


Kwa mujibu wa DKt Mhede  Serikali ipo mbioni kuboresha miundombinu ya usafiri ya mabasi yaendayo kwa haraka kwa upande wa Kibaha na maeneo mengine ambayo mabasi hayo yameanza kutoa huduma.


"Tunakiri bado kuna uhitaji mkubwa wa mabasi kwa mkoa wa Dar es Salam peke yake japo ina magari mengi binafsi lakini inayoa asilimoa kumi tu ya mahitaji ya usafiri na asilimia 90 wanategemea usafiri wa umma" alisema


Msimamizi wa Kitengo cha Kaizen kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Jane Lyatuu alisema mafunzo yanayotolewa na kitengo hicho kwa watendaji wa sekta ya Usafirishaji  DART na  UDART yametolewa kwa wiki saba na yatakuwa endelevu.


Meneja upangaji ratiba na udhibiti kutoka kampuni ya mabasi yaendayo kasi UDART Daniel Madili alisema kupitia mafunzo hayo wanakwenda kufanya maboresho kwenye huduma zao kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Pages