Na Fredy Mgunda, Iringa
JUMLA ya wananchi 3600 wanategemea kunufaika na mradi wa Nyololo Animal Gift Project unaofadhiliwa na world vision Marekani na kutekelezwa na world vision Tanzania wilayani Mufindi mkoani Iringa wenye lengo la kuinua Kipato na kuboresha maisha ya wananchi.
Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo, Meneja wa Kanda ya Iringa wa World Vision Tanzania, Vicent Kasuga alisema kuwa mradi huo utaghalimu kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kwa wananchi wa vijiji saba (7) vya wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Kasuga alisema kuwa lengo la
mradi huo ni kuboresha mnyololo wa thamani kwa kutoa aina tatu (3) za mifugo
ambazo ni Ng’ombe wa Maziwa,kuku na Nguruwe na aina mbalimbali ya mazao ya
bustani kwa ajili ya uboreshaji wa lishe kupitia makundi ya mbogamboga na
matunda kama vile Parachichi, pasheni, chainizi,
Alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kitatumika kununua Ng’ombe wa maziwa mia tatu (300),Nguruwe 600 na kuku 400 kwa kipindi chote cha mradi na watu 1200 wanatarajiwa kunufaika moja kwa moja na wengine 2400 (indirect Participants) watanuafaika na mradi huo.
Kasuga alisema kuwa mradi huo utashirikisha wataalamu wa kilimo na mifugo,viongozi wa serikali ngazi ya kata na vijiji kuwatambua wanufaika wa mradi ambao watakuwa na sifa ya kusimamia na kuendesha miradi ya ufugaji wa Ng’ombe,kuku na Nguruwe kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa.
Aidha Kasuga alisema kuwa mradi huo lazima ujenge misingi bora ya kuinua kipato kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine, kwa kuhakikisha mchango kwenye ulinzi wa mtoto kwa kupunguza ama kuondoa kabisa kunyanyaswa kwa watoto.
“Tumekuwa na mkakati wa kimataifa kwenye jambo la ukatili kwa watoto,hasa ndoa za utotoni kwa kuwa umekuwa ukatili unaofanywa kwa muda mrefu sasa,watoto wengi wamekuwa wanatumikishwa na kuasahau shule ni lazima tutokomeze ukatili dhidi ya watoto,” alisema Kasuga.
Katika wilaya ya Mufindi shirika la World Vision Tanzania limeanza kufanya kazi rasmi mwaka jana (2021) likiwa na jumla ya miradi ya maendeleo yaani Area Programms 3 mmojawapo ni huu wa Nyololo ambao unatekeleza miradi ya maji, Usafi, Afya, Lishe, Elimu na uongezaji wa kipato.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa wananchi na wanufaika wa miradi ya World Vision Tanzania wanapaswa kutoa ushirkiano wa kutosha na kuitunza miradi ili kuleta manufaa kwa wananchi wote.
Mtambule alisema kuwa mradi huo unakwenda kutatua tatizo la lishe kwa wananchi wa wilaya hiyo na kuwaondolea udumavu ambao umekuwa unawatesa sana wananchi wa wilaya hiyo.
Alisema kuwa mwananchi yoyote atakae jitokeza kuuharibu mradi huo serikali itawachukulia hatua kali za kisheria ili kudhibiti uharibifu wa miradi na kusaidia wananchi kunufaika na mradio huo.
Naye meneja wa shamba la mifugo Sao Hill Thomas Tegulo alisema kuwa Ng’ombe hao watasaidia kuinua kipato cha wananchi kwa kuwa wanyama hao wanatunzwa kwa viwango vya kimataifa hivyo wanufaika watapata Ng’ombe bora ambae atakupa faida kubwa.
Tengalo alisema kuwa wamekuwa wanauzoefu wa kufuga wanyama hao kwa ubora unaotakiwa kwa kufanya mnyama huyo kutoa maziwa mengi ambayo yatakuwa na faida kwa wananchi ambao wanafuga wanyama hao.
No comments:
Post a Comment