HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2022

CAG: WANAUME 56 WALIPATA HUDUMA ZA UPASUAJI ZA KUJIFUNGUA


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani),wakati akiwasilisha ripoti yake kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2020/ 2021.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

RIPOTI ya Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere imesema kuwa mapungufu ya udhibiti kwenye Mfuko wa madai ya Bima ya Afya yanaonesha madai ya wanaume 56 walipata huduma ya upasuaji au za kawaida za kujifungua wakati huduma hizo zinatolewa kwa wanawake.

Pia wanachama 444 walipata huduma ya kuchunguzwa picha kamili ya damu ( full blood picture), zaidi ya mara moja kwa siku hadi mara 30 kwenye kituo kimoja.

Akizungumza jijini hapa leo April  12, 2022,  na waandishi wa habari wakati akiwasilisha ripoti yake ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2020 /2021 CAG Kichere amesema kuwa kuwapo kwa malipo ya madai yaliyorudiwa pamoja na madai yanayoonesha wanachama wa  Mfumo wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), walipokea miwani ya kuzomea zaidi ya mara moja wakati utaratibu unaruhusu kutoa miwani mara moja kwa mwaka.

Mdhibiti huyo ameongeza kuwa udhaifu huo umesababishwa na kukosekana kwa udhibiti katika mfumo wa madai  iliyosababisha hasara ya shilingi milioni 14.41 katika mfuko.

" Ninapendekeza Mfuko wa Bima ya Afya kurejesha kiasi kilichopotea kutoka kwa watoa huduma za afya husika,kuboresha mfuko wa madai w CMIS ili kuhakikisha unasaidia maafisa wanaohusika kuangalia uhalali wa madai yaliyowasilishwa.

No comments:

Post a Comment

Pages