HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 17, 2022

HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA KUTUMIA SH.BILIONI 1.6 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SEKTA YA AFYA

Wananchi wa Kata ya Makuro katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida wakitoka kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata hiyo wakati Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge alipofanya ziara ya siku moja ya kukagua ujenzi hicho jana.
Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Vicent Ngunda na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge wakiongoza kukagua kituo hicho cha Afya.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge akihutubia wananchi wa kata hiyo baada ya kukagua kituo hicho cha afya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Eliya Digha akizungumza katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika baada ya ukaguzi wa kituo hicho cha Afya.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri akizungumza kwenye mkutano huo.




Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya.

Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Vicent Ngunda akielekeza jambo kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo ya Ilongero.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Makuro, Moses Daniel akitoa taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha kata hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wakifurahia kujengewa kituo cha Afya.
Safari ya ukaguzi wa kituo hicho cha Afyaikifanyika.
Ukaguzi wa kichomea taka cha kituo hicho cha Afya ukifanyika.
Ujenzi wa majengo mengine ya kituo hicho ukiendelea.


Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Vicent Ngunda akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dk.Binilith Mahenge (katikati) na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Paskas Mulagiri wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo.
Muonekano wa majengo ya Kituo cha Afya cha Kata ya Makuro.


Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara baada ya kufanyika ukaguzi wa kituo cha Afya cha Makuro.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ilongero.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge akiwaelekeza jambo wajumbe waliokuwepo kwenye ziara hiyo baada ya ukaguzi huo.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida


HALMASHAURI ya Wilaya ya Singida kutumia Sh. Bilioni 1.6  kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya sekta ya Afya wilayani humo.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ester Chaula wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge kaztika ziara yake ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya jana.

Miradi iliyokaguliwa na Dk.Mahenge ni ujenzi wa Kituocha Afya cha Kata ya Makuro ambao utagharimu Sh.500  Milioni ambapo kwa awamu ya kwanza walipokea Sh.250 Milioni na Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ilongero ambao ujenzi wake umefikia hatua ya uwekekaji wa mfumo wa umeme na upakaji wa rangi majengo.

Chaula alisema fedha hizo zimegawanyika katika maeneo manne ambapo katika miradi ya Afya na Usafi wa Mazingira wametenga Sh. 281.5, mradi wa boresha afya kwa tozo ulitengewa Sh.500 Milioni kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya cha Kata ya Makuro na Sh.77 Milioni kwa ajili ya UVIKO 19.

Aidha Chaula alisema walipokea Sh.800 Milioni kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili za wagonjwa na chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Ilongero ambao ujenzi wake upo hatua za mwisho kukamilika.

Alitaja fedha zingine walizopokea kuwa ni Sh.340  ambazo zitatumika kujengea nyumba moja ya watumishi ambayo zitaishi familia tatu na ujenzi wa chumba cha wagonjwa mahututi.

Akizungumzia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Makuro alisema fedha walizopokea awamu ya kwanza zimetumika kujengea jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Maabara na kichomea taka na  kuwa Sh. 250 zilizotolewa awamu ya pili zitatumika kujengea jengo la Mama na Mtoto, Chumba cha Upasuaji na Chumba cha kufulia.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge akizungumza na Wananchi wa Kata ya Makuro baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kituo hicho cha afya alisema katika kipindi cha mwaka mmoja Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mkoa wa Singida pekee imetoa Sh.232 Bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Serikali yetu inayowajali wananchi wake katika kipindi cha mwaka mmoja imetoa Sh.232 Bilioni na kati ya fedha hizo kwa mkoa mzima vinajengwa vituo vya afya 15 kwa wakati mmoja kikiwepo na hiki cha Kata ya Makuro na Hospitali za wilaya mbili hii hapa ya Ilongero na ile ya Wilaya ya Ikungi hii sio kazi ndogo anayoifanya Rais wetu tuna kila sababu ya kumpongeza" alisema Mahenge.

Dk. Mahenge alitumia nafasi hiyo kuwapongeza viongozi wote wa chama na Serikali, Watumishi  pamoja na Wananchi wa Wilaya hiyo kwa kusimamia vizuri fedha zilizotolewa na Serikali katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa makini na uaminifu.

No comments:

Post a Comment

Pages