HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 06, 2022

MKURUGENZI UTURN COLLECTION AFIKISHWA KIZIMBANI

MKURUGENZI wa mtandao wa kijamii wa Uturn Collection, Allen Salum Mhina (31), mkazi wa  Temeke, mtandao huo wa Uturn collection na Mange Kimambi App, zimeshtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa matatu likiwemo la kuchapisha maudhui yanayokiuka haki na uhuru wa mtu mwingine.

Mashtaka mengine waliyosomewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate ni kufanya kazi ya uandishi wa habari bila kuwa na kibali na kutoka bodi ya ithibati ya wanahabari na kumfedhesha mtu kwa njia ya mtandao (cyber Bullying)

Hata hivyo upelelezi katika kesi hiyo namba 57 ya mwaka 2022 umeishakamilika na mshtakiwa Mhina anatarajiwa kusomewa maelezo ya awali (Preliminary Hearing) Aprili 27, 2022

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali waandamizi Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Sylivia Mitanto imedai Machi 9, 2022 katika maeneo tofauti ndani na nje ya nchi ya Tanzania washtakiwa walichapisha video ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha wagonjwa Mahututi ( ICU) maudhui ambayo yanadhuru haki ya faragha ya mgonjwa (Profesa Jay)

 Katika shtaka la pili inadaiwa kuwa katika tarehe tofauti kati ya Septemba 22,2022 na Machi 14,2022  huko Kinondoni eneo la Manyanya  katika Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam mshtakiwa Allen na kampuni ya Uturn collection walifanya kazi ya uandishi wa habari bila ya kuwa na kibali kutoka bodi ya ithibati ya wanahabari.

Katika shtaka la tatu inadaiwa, Machi 9, 2022 katika maeneo tofauti ndani ya nje ya nchi ya Tanzania, mshtakiwa Allen kupitia mfumo wa kompyuta unaojulikana kama Mange Kimambi APP,  unaosimamiwa na Uturn Colection alichapisha video ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha wagonjwa Mahututi ( ICU) kwa nia ya kusababisha emotional distress.

No comments:

Post a Comment

Pages