Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kusimamia mifumo ya kuzuia vitendo vya kiuhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Katika hatua hiyo Jeshi limewakamata watu wawili (2) waliokuwa wanajaribu kuharibu kwa kukata baadhi ya vyuma vya ngazi moja ya nguzo namba P9 ya Daraja la Tanzanite lililopo maeneo ya Salender, Ilala.
Watuhumiwa hao ambao majina yao (yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) walikamatwa tarehe 02/04/2022 saa 10 alfajiri wakiwa wanajaribu kufungua vyuma vilivyopo kwenye nguzo ijulikanayo kama P9 ambayo ipo kwenye daraja hilo. Wanahojiwa kwa kina na watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa hatua zaidi.
Pia Jeshi la Polisi limewakamata watu wengine kumi (10) waliokutwa chini ya Daraja huku wakidai wanaokota vyuma chakavu kwa ajili ya biashara ya vyuma. Watuhumiwa hao pia wanahojiwa kwa kina ili kubaini malengo yao kwa ujumla chini ya Daraja hilo yalikuwa ni nini na kuona kama wanamahusiano na wale waliokuwa wanajaibu kuiharibu baadhi ya miundombinu ya nguzo ya daraja hilo.
Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kuwa halitamvumia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma, Ulinzi katika eneo hilo na maeneo mengine umeeendelea kuimarishwa na atakayejaribu kuiharibu atakamatwa na mifumo ya kisheria ya kishughulika nae itazingatiwa.
No comments:
Post a Comment