HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 09, 2022

Sensa ya watu, makazi kuanza Agosti 23

Na Irene Mark

RAIS Samia Suluhu Hassan ametangaza rasmi kuwa Agosti 23,2022 ndio siku ya kuanza zoezi la sensa ya watu na makazi.

Akizindua nembo na tarehe ya kuanza kwa zoezi la sensa hiyo kitaifa, leo Aprili 8,2022 Rais Samia amewataka wananchi wote kujitokeza kushiriki zoezi hilo huku akisisitiza kwamba ni kosa kisheria mtu kukataa kuhesabiwa.

“Tuache dhana kwamba kuhesabiwa ni nuksi tunahewabiwa ili kupanga maendeleo yetu. Tushiriki sote kwenye zoezi hili tusiwafiche watoto wetu hasa wenye ulemavu,” amesisitiza Rais Samia.
 
Uzinduzi huo uliofanyika visiwani Zanzibar, Rais Samia amesema ana imani kubwa ya kufanyika kwa sensa bora ya watu na makazi kuliko zilizopita huku akikumbusha kwamba baada ya kupata uhuru wa Tanganyika na baadae Tanzania, sensa ya kwanza ilifanyika mwaka 1967.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wakuu wa kitaifa wa Tanzania Bara na Zanziba, viongozi wa vyama vya kisiasa, dini, mabalozi wa nchi mbalimbali na asasi za maendeleo.


 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambapo itaanza kutumika baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Nembo ya vyeti maalum kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Sensa, kuashiria kumpa Jukumu la kuanza kazi hiyo rasmi wakati wa  uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itaanza kutumika, baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua rasmi Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itaanza kutumika rasmi, baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SC Johnson ya nchini Marekani Bw. Fisk Johnson Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar leo tarehe 23 Agosti 2022. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SC Johnson ya nchini Marekani Bw. Fisk Johnson na Ujumbe wake baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar leo tarehe 23 Agosti 2022. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.
 

 

No comments:

Post a Comment

Pages