HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 20, 2022

WAFANYABIASHARA DODOMA WATISHIA KUANDAMANA

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema zoezi la kuwaondoa  wafanyabishara wadogo (wamachinga) wa soko la matunda na Mbogamboga Sabasaba kupisha ukarabati wa soko hilo lazima uhakiki madhubuti ufanyike ili kila mfanyabiashara apate haki yake.

Mafuru amebainisha leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kutokana na baadhi ya wafanyabishara katika soko la sabasaba kuendelea kuwa na wasiwasi juu ya pangua pangua ya wafanyabishara katika soko hilo kupisha ujenzi.

Hivyo Mafuru amefafanua kuwa lengo la Jiji ni kuboresha mazingira ya wafanyabishara na si kuwadhulumu.

Hatua hiyo imekuja baada ya wafanyabiashara wa soko la Sabasaba jijini Dodoma kutishia kuandamana kwenda bungeni kumuona Waziri mkuu Kassim Majaliwa ili kumfikishia kilio chao cha kuondolewa bila kushirikishwa mkurugenzi wa jiji hilo.

Amesema lengo ni kufanya uhakiki na  kuwatambua nani anamiliki nini na anafanya nini  watarudi katika maeneo yao .

Aidha amesema soko hilo ni la historia na limechakaa na ni la muda mrefu tangia mwaka 1996 halijafanyiwa ukarabati miundominu yake ni mibovu .

"Dodoma Sasa ni Jiji na ndiyo Makao Makuu ya nchi na soko la Sabasaba limekuwa likilisha karibu Wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma na ndio maana tunataka kufanya ukarabati .

Aidha Mkurugenzi huyo wa Jiji la Dodoma wamesema wapangaji waliojimilikisha zaidi ya kibanda kimoja watamiliki kibanda kimoja tu ili kuwapa nafasi watu wengine kwani kuna baadhi ya wafanyabishara wamejimilikisha zaidi ya kibanda 20 na kuvipangisha kwa watu wengine kwa bei ya Juu.

Amesema jiji halina lengo la kuwaonea wafanyabiasahara bali kinachotakiwa ni kuwashirikisha kila hatua ili kuweza kupata uelewa wa pamoja na kila mtu kuridhika na maamuzi hayo.

Hata hivyo amesema malalamiko ambayo wamekuwa wakiyapata yanaonyesha kuwa wafanyabiashara hao hawana imani na jiji katika kutekeleza mpango huo.

Amesema ili kupata kauli moja wanapanga kuendelea na vikao vya kujadilina baina ya jiji na uongozo wa soko hilo ili kupata namna bora ya kufikia mwafaka.

Kwa Upande wake Afisa Biashara ya Jiji la Dodoma Domitila Vedasto amesema lengo la kuwahamisha kwa muda wafanyabiashara ni kupisha uboreshaji wa miundo mbinu soko la sababsa lina historia ya muda mrefu tangu mwaka 1996 waliahamishwa kutoka Nyerere Square na kupelekwa maeneo mbalimbali.

Pia amesema Soko la sababasa miundombini yake imechakaa na hata ukienda sasa hivi kuko wazi lakini pia hili ni jiji na makao makuu hatuwezi kuwa na soko la aina ile  kama jiji tukasema kuwe na kitu cha kufanya kuboresha soko kama hadhi ya jiji na kuendana na makao makuu ya nchi.

"Tukawaza kuweka mkakati kwa maana katika mradi huu tutanza ujenzi mwezi wa saba na  huwezi kuanza bila kuwashirikisha wadau ,vikao vimeanza tangu mwaka jana kuhusiana na changamoto kikubwa miundombinu vikao vya kuanza kujenza tumeanza mwezi wa kwanza wtaalam walikuja tukawashirikisha," amesema Afisa Biashara .

Naye Mkuu wa idara ya Fedha Jiji la Dodoma Rahabu Philip, alisema siyo kweli kuwa wafanyabiashara hao hawajashirikishwa katika mpango huo wa jiji.

Rahabu amesema mpango wa ukarabati wa soko la sabasaba ni wa kitambo lakini hakutekelezwa kwa wakati kutokana na ufinyu wa bajeti uliokuwepo.

Ikumbukwe kuwa katika mkakati wa uboreshaji wa soko la sabasaba march 4 2022 Mkuu wa mkoa wa Dodoma kuwaoredhesha wafanyabishara wote katika mfumo maalum ili kuweza kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza hapo baaadae ambapo mkakati wa Jiji ni ujenzi wa soko jipya sabasaba litakaloweza kuhudumia zaidi ya wafanyabishara elfu Saba.

Mwishoni mwa wiki iliyopita viongozi wa soko hilo wakizungumza na waandishi wa habari walidai kuwa wanapanga kufanya maandamano hadi Bungeni ili kufikisha kilio chao kwa waziri mkuu.

No comments:

Post a Comment

Pages