HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 07, 2022

KAMANDA MFINANGA: MATUKIO MENGI YA MOTO WAOPIGA SIMU YA MSAADA NI WAPITA NJIA NA MAJIRANI


Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Kambanda wa Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Julishaeli Mfinanga akielezea namna wanavyofanya kazi za uokoaji katika Mkoa huo.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

KAMISHNA  Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji ambaye pia ni Kamanda wa Zima Moto na Uokaji Mkoa wa Dodoma Julishaeli Mfinanga amesema kuwa  changamoto wanayokutana nayo katika uokoaji ni ucheleweshwaji wa taarifa za tukio husika kwa kuwa  aliyeunguliwa huanza kupambana mwenyewe badala ya kutoa taarifa kwa wakati.

Kamanda Mfinanga  ameyasema hayo jijini hapo jana  katika kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Mzima Moto ambayo huadhimishwa Ulimwenguni kote  Mei, 4 kila mwaka baada ya nchi ya Australia kupoteza askari wake mwaka 1999 kutokana na janga la moto wakati wanapambana na tukio la moto huo msituni ambao ulipoteza mwelekeo na kuwageukia askari hao amesema mtu huyu atakaposhindwa kuukabili moto ndipo anakumbuka kupiga simu.

Amesema kuwa kwa tafiti walizozifanya ya matukio ya moto aliyeunguliwa siye anayepiga simu wanaotoa taarifa za kutaka msaada wa kusaidiwa kuokolewa ni majirani au mpita njia.

" Aliyepatwa na tukio anapatwa na mshtuko hakumbuki hata kupiga simu ya dharura  na wakati mwingine hakumbuki hata simu yake alipoiweka ili apige mpita njia au jirani ndiye anapiga simu na kutoa taarifa," amesema.

Amesema kuwa jeshi hilo halijawahi kuchelewa katika eneo la tukio la uokoaji na kwamba wakipata taarifa kwa wakati inawasaidia kufika haraka kwenye eneo la tukio.

Kamishna huyo amefafanua kuwa magari ya zima moto yanauwezo mdogo wa kubeba maji na sio Tanzania tu bali hata nchi za nje hivyo magari yote ya Zima moto kwa yenye uwezo wa juu kabisa  hayazidi lita 16,000 za maji na  kwa nchi zilizoendelea wanatumia bomba la maji 'ire hydrant' kuweza kukamikisha tukio la uokoaji.

"Wenzetu nchi zilizoendelea wakifika katika eneo la tukio hawawezi kuondoka wanahakikisha  tatizo wanakimaliza,
kumekuwa na malalamiko kwamba  tunafika  eneo la tukio hatuna  maji. Tunafika kwa wakati na tukiwa na maji tatizo magari yana uwezo mdogo wa kubeba  maji lifa 6000 hadi 7000 zinaisha kwa haraka" ameeleza.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mnadani Joyce Kaishozi amesema kuwa  elimu ya zima moto wanaitoa shuleni hapo na kwamba kitabu chao cha  Uraia na maadili cha darasa la Saba kina mada ambayo ni Elimu ya zima moto na uokoaji katika jamii.

Mwalimu huyo amefafanua kuwa kitabu hicho kinaeleza hatua za uzimaji moto na  uokoaji na kwamba jeshi hilo limeenda sehemu sahihi ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Amesema kuwa shule hiyo ina walimu 32 Wanawake 31 na wakiume ni mmoja elimu ya zima moto inatolewa shule hapo kwa nadharia.

"Tumefurahi Sana kupata ugeni huu wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya mzima moto, umekuja sehemu sahihi ambayo tunafundisha na ugueni huu usiwe siku za kilele tu mje mtoa elimu zaidi ya Uokoaji," amesema Mwalimu Joyce.

Aidha Mwalimu Joyce ameiomba serikali kuongeza vifaa vya zima moto na uokoaji kwa kuwa jiji hilo awali lilikuwa Manispaa na sasa ni  jiji tena makoa makuu ya nchi ambapo wakazi wengi wanaongezeka.

Akitoa Elimu ya uokoaji  Afisa Habari  Uhusiano na  Elimu kwa Umma Sajenti Joyce Kapinga  amesema kuwa wanamajukumu mbalimbali katika jamii ya uokoaji  kama vile majanga ya moto, majini ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya afya kwa jamii hiyo.

Ameongeza kuwa wanatoa elimu ili kuondoa ujinga na kuweza kuzuia moto  usitikee na kuleta majanga katika jamii iliyowazunguka.

Mkoa wa Dodoma umeadhimisha Maadhimisho hayo katika Shule ya msingi Mnada, Soko la Mavunde lililopo Chang'ombe na Kiwanja cha Ndege kwa kutoaka elimu ya zima moto na uokoaji na Chingangali Park ambapo askari wa jeshi hilo walitoa elimu ya uokoaji wa mtu aliyezama ndani ya maji na yule aliyepoteza maisha akiwa ndani ya maji.

No comments:

Post a Comment

Pages