Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Mpango akikabidhi Cheti kwa Mkuu wa Idara ya Ubunifu wa Benki ya NMB, Josina Njambi na Mkuu wa Idara za Serikali na Ofisi ndogo za Makao Makuu Dodoma wa NMB, Vicky Bishubo kwa kutambua mchango wa benki hiyo kwa kuendeleza shughuli za ubunifu, wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa, iliyofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na kulia ni Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia-Profesa Adolf Mkenda.
Maafisa wa NMB katika picha ya pamoja wakati
wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa, iliyofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Philip
Mpango ameikabidhi Benki ya NMB cheti cha kutambua mchango wa benki hiyo
katika kuendeleza shughuli za ubunifu nchini, ikiwa ni pamoja na
kudhamini wiki ya ubunifu kitaifa.
Cheti hicho kilikabidhiwa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki
ya Ubunifu Kitaifa yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
jana na kupokelewa na Mkuu wa Idara ya Ubunifu wa Benki ya NMB – Josina
Njambi pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma
za Serikali na Ofisi ndogo za Makao Makuu Dodoma – Vicky Bishubo.
Aidha, kabla ya kukabidhi cheti hicho, Makamu wa Rais, Mhe Dkt.
Mpango alitembelea banda la NMB ambapo Josina alimueleza kuhusu fursa
ambayo benki ya NMB imewaletea wabunifu kupitia mfumo wa NMB Sandbox
Environment.
“Tumekuja na mfumo huu wa majaribio kwa ajili ya Vijana wabunifu
wenye suluhishi za kifedha kujaribu masuluhisho yao kisha kuwasaidia
wabunifu hao kuingia sokoni,” alisema Josina.
“Mpaka sasa wapo wabunifu zaidi ya 150 ambao wanaendelea kufanya majaribio ya suluhishi zao katika mfumo huu.”
No comments:
Post a Comment