HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 28, 2022

OWA, EAAW Tanzania wajitokeza kutetea kuku


Na Mwandishi Wetu


HADI kufikia Aprili 2022, asilimia 88 ya kampuni zilizotoa ahadi ya matumizi ya mayai yatokanayo na ufugaji huria ya mwaka 2021 zimetimizwa.
 
Wakati huohuo, mashirika 2,300 ya chakula kote ulimwenguni yamepitisha sera za ustawi wa wanyama ambazo huondoa vizimba vinavyotumia betri kutoka kwenye mnyororo wao wa usambazaji na matumizi ya mayai.

Kati ya ahadi hizo, kampuni 982 zimekamilisha kwa ufanisi ubadilishaji wa mnyororo wao wa ugavi bila kizuizi.
 
Hayo yalibainika Mei 16, 2022 wakati Shirika linalotetea haki za wanyama, Open Wing Alliance (OWA) lilipozindua ripoti ya utimilifu wa ufugaji huru ya mwaka 2022.

Hii ni ripoti ya pili ya utimilifu wa mayai yatokanayo na ufugaji huria, ambayo inaarifu juu ya kujitolea bila malipo kwa biashara kimataifa.

Ripoti hii inatoa fursa kwa kila kundi na umma kuelewa kwamba makampuni mengi yanatimiza ahadi zao za ustawi wa wanyama, lakini kuna baadhi ya makampuni yanarudi nyuma linapokuja suala la maendeleo na uwazi.
 
Muungano wa The Open Wing Alliance (OWA) duniani kote, unafanya kazi bila kuchoka kukomesha matumizi ya kikatili ya kuwafungia kuku wanaotaga na kuingiza mayai ndani ya mfumo wetu wa chakula hasa viwandani.
 
Huu ni muungano wa zaidi ya mashirika 80 kutoka nchi 63 ambayo yanayofanyakazi kwa zaidi ya muongo mmoja ili kupata ahadi ya kukomesha ukatili dhidi ya kuku kutoka kampuni kubwa zaidi za chakula duniani.

Tanzania haiko nyuma katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanyama, OWA imekuwa ikishirikiana na mashirika mbalimbali ya ustawi wa wanyama, miongoni mwao ni shirika la Education for African Animals Welfare (EAAW), katika kutekeleza shughuli zake hasa utoaji wa elimu na kampeni zinazolenga kukomesha ukatili dhidi ya wanyama hususan kuku waliofungiwa kwenye vizimba.

Kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2022 kumekuwa na makubaliano ya kisera ya kukomesha ukatili dhidi ya kuku na kitiwa saini zaidi ya 500 na mashirika mbalimbali kote ulimwenguni, wakati barani Afrika tuna ahadi 15 tu za mashirika yanayokubaliana na ukomeshaji wa ukatili dhidi ya kuku.
 
Kuna baadhi ya mashirika ambayo yana sera ya kuondoa matumizi ya vizimba katika mnyororo wao wa ugavi na kufikia asilimia 100 ya mayai yatokanayo na kuku wasiofugwa kwenye vizimba na hawajaweka wazi maendeleo yaliyofikiwa katika maeneo yao.

Miongonu mwa makampuni hayo ni pamoja na Hilton Hotels, Radisson Hotels Group na Unilever.

Hata hivyo, barani Afrika kuna mashirika yaliyofikia na kutimiza ahadi ya uondoaji vizimba katika ufugaji wa kuku, ambayo ni Danone, Marriott, Starbucks na Kraft Heinz ambao wanaripoti kwa uwazi juu ya maendeleo yao.

Mashirika hayo yanahimiza wengine ambao bado kufanya bidii katika utekelezaji wa sera ya ufugaji huria.

Mapema mwaka huu, kampuni ya kimataifa ya Majid Al Futtaim ambao ni wauzaji wakubwa wa mazao ya kuku kupitia maduka ya Carrefour nchini Kenya, Kameruni, Uganda na Misri walitoa ahadi ya sera ya kimataifa ya kutofungamana na wauzaji mayai kutoka kwa wafugaji wanaotumia vizimba.

Majid Al Futtaim aliangazia watumiaji wa mayai katika eneo hilo wanajali ustawi wa wanyama.

Hata hivyo bado kuna changamoto kwa ustawi wa kuku katika ukanda wa Afrika na kuna makampuni mbalimbali ambayo yako nyuma katika kukubaliana na sera ya uondoaji vizimba na hayajatoa ahadi zao kukomesha ukatili huo.
 
Wauzaji wa reja reja kama vile Pick n Pay, Shoprite na Massmart wamelegalega na kurudi nyuma katika maendeleo haya ya ustawi wa kuku wa mayai katika ukanda wa Afrika na wanahitaji kujitolea zaidi katika kusisitiza ufugaji bila vizimba ili kudhihirisha kwa umma kwamba wanajali ustawi wa wanyama.

Mkurugenzi wa OWA, Alexandria Beck anasema, "Kupata maelfu ya ahadi katika sera ya ustawi wa wanyama ni kiashiria muhimu cha maendeleo kwa wanyama wanaofugwa kwa ajili ya chakula, ingawa tunajua kwamba ahadi pekee hazitasababisha kuboreshwa kwa hali za wanyama.
 
"Ili kuwaokoa kuku kutokana na maisha ya ukatili ya kufungiwa kwenye vizimba vya chuma, tunahitaji kuona makampuni yakitengeneza na kutoa taarifa juu ya maendeleo kuelekea malengo yao ya ufugaji huria”.

Kwa mujibu wa Beck, takwimu zinaonesha kwamba siku zijazo hakutakuwa na ufugaji wa vizimba kwa zaidi ya  asilimia 11 ya kuku duniani kote.
 
Taarifa hii ni kwa mujibu wa OWA kwa kushirikiana na EAAW la Tanzania.
 

No comments:

Post a Comment

Pages