HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 07, 2022

Wafanyakazi wa PURA washiriki sherehe za Mei Mosi 2021

 

Baadhi ya wafanyakazi wa PURA wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya Silku ya Wafanyakazi, Mei Mosi 2022 kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 

Wafanyakazi wa PURA wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi Kitaifa 2022, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. 

 

 

Na Janeth Mesomapya



Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli
(PURA) wameungana na maelfu ya Watanzania kufanya maandamano
ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani leo Mei 1, 2022.

Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu
isemayo mishahara na 'maslahi bora kwa wafanyakazi ndiyo kilio chetu,
kazi iendelee’.

Akizungumzia maadhimisho hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu na
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi PURA, Mhandisi Charles
Sangweni amesema maadhimisho hayo ya Siku ya Wafanyakazi kwa
mwaka huu ni ya sita kwa PURA kushiriki tangu kuanzishwa kwake
mwaka 2015, na katika kipindi hiki imeshuhudiwa kasi ya kuimarika
kwa taasisi hii ikiwa ni pamoja na ongezeko la watumishi na ufanisi
katika utekelezaji wa shughuli za Mamlaka.

“Siku ya Mei Mosi ni muhimu kwetu watumishi wa PURA na
watumishi wote duniani, kwani ni siku inayotukumbusha wajibu wetu
wa kutumikia wananchi kwa uadilifu, kwa umoja, ufanisi na kwa haki
inayostahili,” aliongeza.

Mhandishi Sangweni pia ametoa rai kwa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo
kuendelea na moyo wa kujituma na kuongeza ufanisi katika utendaji
kazi ili kuleta matokeo chanya.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya
(TUGHE) kwa tawi la PURA, Bw. Abbas Kisuju amesema PURA
imeungana na taasisi nyingine kwenye maandamano hayo ikiwa ni njia
ya kutambua mchango wa watumishi kwenye utekelezaji wa majukumu
ya Mamlaka hiyo.

“Hii pia imekuwa fursa kwetu kuungana na wafanyakazi wa taasisi
nyingine ili kubadilishana mawazo kuhusu utatuzi wa changamoto
mbalimbali tunazokabiliana nazo kwenye maeneo yetu ya kazi,”
aliongeza.

PURA imeshiriki kwenye maadhimisho hayo kwa wafanyakazi wa ofisi
zake za Dar es Salaam na Dodoma kushiriki maadhimisho yaliyofanyika
Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Pages