HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 19, 2022

TCRA kutoa masafa na namba maalum bure kwa watafiti

Wanafunzi wakiwa katika Banda la TCRA katika Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayoendelea jijini Dodoma.
 
 

Afisa  Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Aika Benson akimpa maelezo ya shughuli za mamlaka kwa mteja aliyetembelea maonesho ya Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma.

 

Afisa Mkuu  Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akimpa maelezo ya shughuli za mamlaka kwa mteja aliyetembelea maonesho ya Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma.

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatoa masafa pamoja namba maalum za kutoa  huduma  bure kwa watafiti  wote watanzania wanaofanya tafiti zinazolenga katika kutumia Teknolojia ya mawasiliano kuongeza tija katika shughuli mbalimbali nchini.

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya Ubunifu nchini yanayofanyika mkoani Dodoma Afisa Mkuu wa  Mawasiliano na Mahusiano wa TCRA  Mabel Masasi amesema utaratibu huo unalenga katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha ufanyaji wa tafiti ambazo zinalenga katika kuleta maendeleo nchini.

Akizungmzia jinsi ya kupata masafa na namba kwa ajili ya utafiti  Mabel amesema iwapo watafiti  wanafanya utafiti kupitia vyuo basi vyuo vyao vinatakiwa kuwasiliana na Mamlaka hiyo ili kuweza kukamilisha taratibu za kupata masafa au namba ya kufanyia utafiti bila kulipia.

Kuhusu watafiti binafsi  wanaotaka kufanya  utafiti kwa kutumia rasilimali hizo   Mabel amesema watafiti binafsi  watatakiwa kwenda kujisajili Costech  ambapo kupitia wao wataweza kuombewa rasilimali hizo kwa ajili ya utafiti  bila kulipia.

Madhimisho ya ubunifu hufanyika kila mwaka  ambapo kauli mbinu ya mwaka huu ni Ubunifu kwa maendeleo endelevu.

No comments:

Post a Comment

Pages