“Uhuru wa habari na haki ya kujieleza vikitumika vizuri katika taifa ni kitu kimoja muhimu sana katika kulijenga taifa kimaendeleo”
Mhariri wa magazeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ali Haji Mwadini alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na mwandishi wa makala hii na kuelezea kuwa haki ya kujieleza kutokana na umuhimu wake imetajwa katika Ibara 14 ya katiba ya Zanzibar.
Kwa upande wa uhuru wa habari Mwadini alieleza kuwa Sheria za habari zinatakiwa ziwe rafiki na ziangalie mazingira na zinaendana na wakati wa sasa.
“Rais wetu wa Zanzibar ameonekana wazi wazi kwa nyakati tofauti kuwambia wahusika wazipitie sheria za habar ili ziendane na wakati tulionao” alieleza Mwadini.
Katika kuhakikisha uhuru wa habari na haki ya kujieleza unasismama katika visiwa vya Zanzibar, shirika la Inernews Tanzania wakishirikiana na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania kwa upande wa Zanzibar (TAMWA-ZNZ)
Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa alisema anamamini madai ya uwepo sheria mpya sasa unaweza kupatikana kutokana nia njema zinazonyeshwa kwa jamii na Serikali.
“Jamii na Serikali kwa ujumla wanapaswa kufahamu kuwepo kwa sheria mpya ya habari kutaongeza usawa na uwajibikaji katika kila jambo na kupelekea kuchochea watu kuwajibika hivyo kuwa sehemu ya chanzo kikubwa cha maendeleo ndani ya Zanzibar” alieleza Dk. Mzuri.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Suleiman Abdulla Salim wakati wa kuadhimisha Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa upande wa Zanzibar alisema Wanatasnia ya Habari muda wote wahakikishe wanazingatia Maadili ya Utangazaji nchini ikiwa ni pamoja na Ukweli wa habari, mezania, kuepuka kuharibu majina ya watu na kulinda Amani na Utamaduni wa Mzanzibari usiharibiwe.
Kaoli hiyo ilikuwa inatamalaki kuwa uhuru wowote wa kujieleza lazima upewe mipaka jambo ambalo wataalamu wengi wamesema ni kinyume uhuru wa habari na haki ya kujieleza.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika kuchagiza na kulinda haki ya uhuru wa maoni na kujieleza Frank La Rue alisema serikali lazima zichangie na kuleta mabadiliko badala ya kukandamiza watu.
Akitoa ujumbe maalumu wa kuadhimisha
siku ya uhuru wa vyomvo vya habari yaliofanyika Mai 3, kwamba hivi sasa matukio
mengi yanajiri Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ambapo watu hususani
vijana kwa pamoja wamesimama kidete ili kupinga miongo ya ukandamizaji na
kunyimwa haki za msingi za binadamu.
La Rue alisema anawapongeza watu hao wakiwemo waandishi wa habari, wanaharakati, kwa ujasiri wao wa kudai mabadiliko, demokrasia, uwazi na haki
Mussa Kombo Bakari ambaye Katibu wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar amesema tume hiyo ipo itayari kushirikiana kwa karibu na wadau wa habari Zanzibar ili kupatikana kwa sheria bora ya habari inayoendana na wakati uliopo sasa.
“Sisi kama tume ya kurekebisha sheria visiwani hapa tutahakikisha tunafanya upembuzi wa kina kila kipengele ambacho kimewasilishwa na wadau kama changamoto ili tuweze kupata kitu ambacho kitakua bora zaidi kwenye sheria mpya” alieleza .
Ni vyema katika kuwa na uhuru wa habari na haki ya kujieleza ni lazima ki8la mmoja kuchukua hatua ili vitu vipatikane kwani katika nchi yoyote kama watu watakaa kimya itakuwa itakuwa vigumu viongozi ama seikali kubadilika ni watu waseme ili wasikilizwe wanachokieleza.
Vyombo vya habari vinajukumu kuwa la kuwapatia wananchi kutoa waliyonayo moyoni ila kwa yale ambayo yanajenga kwa maslahi ya umma.
No comments:
Post a Comment