HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 16, 2022

Wananchi wa Kijiji cha Msomera wahakikishiwa kupata huduma za mawasiliano-Dk.Yonazi

Katibu Mkuu wa  Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jimmy Yonazi (mwenye Suti) akizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Uongozi wa Wilaya Handeni wakati wa akiangalia mnara wa muda wa kampuni ya Airtel wa ajili ya huduma  za mawasiliano  katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani mkoani Tanga kwa ajili wananchi  waliohamishwa  Ngongoro wakati Katibu wa Wizara hiyo alipotembelea Kijiji hicho kuangalia huduma za Mawasiliano.

 

Katibu Mkuu wa  Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Jimmy Yonazi (Mwenye Suti) akiangalia mfumo wa Maji akiwa  Watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Uongozi wa Wilaya Handeni wakati alipofanya ziara  katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga  kwa  wananchi  waliohamia na wageni kutoka Hifadhi ya  Ngongoro wakati Katibu wa Wizara hiyo alipotembelea Kijiji hicho kuangalia huduma za Mawasiliano.

 

Katibu Mkuu wa  Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Jimmy Yonazi (Mwenye Suti) akizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Uongozi wa Wilaya Handeni wakati wa ushushaji wa mnara kwa ajili ya huduma  za mawasiliano  katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani mkoani Tanga kwa ajili wananchi  waliohamishwa  Ngongoro wakati Katibu wa Wizara hiyo alipotembelea Kijiji hicho kuangalia huduma za Mawasiliano.

 

Katibu Mkuu wa  Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Jimmy Yonazi (mwenye Suti), akizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Uongozi wa Wilaya Handeni wakati wa ushushaji wa mnara kwa ajili ya huduma  za mawasiliano  katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani mkoani Tanga kwa ajili wananchi  waliohamishwa  Ngongoro wakati Katibu wa Wizara hiyo alipotembelea Kijiji hicho kuangalia huduma za Mawasiliano.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk.Jabiri Bakari akiangalia mfumo wa maji katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga kwa ajili ya wananchi wanaohamia kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kwa kuanza makazi wakiwa na huduma mbalimbali.

Mnara wa Muda  Kampuni ya Airtel tayari kwa kuanza kutoa huduma ya mawasiliano katika Kijiji cha Msomera ambacho wanahamia wananchi wanaotoka katika Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha ikiwa ni jitihada za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya kukikisha wananchi wanapata mawasiliano.
 

 

Na Mwandishi Wetu

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Jimmy Yonazi amewahakikishia wakazi wa kijiji cha  Msomera  wilayani Handeni mkoani Tanga na wageni watakaohamia kutokea Ngorongoro uhakika wa kupata huduma  bora za mawasiliano wawapo Msomero.

Akizungumza katika ziara ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika kijiji cha Msomera leo Dkt. Yonazi amesema serikali inatambua umuhinu wa mawasiliano katika kukuza uchumi hivyo wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake wamejipanga kuhakikisha mawasiliano hayayumbi.

Dkt Yonazi ameiagiza Mamlaka  ya Mawasiliano TCRA kuhakikisha kuwa inawaelekeza watoa huduma wote wa mawasiliano kwenda kuwekeza na kutoa huduma za mawasiliano kijiji huko ili watumiaji wapate wigo mpana zaidi wa kuchagua.

Akizumgumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano TCRA Dkt Jabir Bakari amesema TCRA itatekeleza agizo hilo mara moja na kuongeza kuwa   katika kuitikia wito wa kuboresha mawasiliano  TCRA ili kuweza kurahisisha huduma ndani ya kijiji na kuweza kufanya biashara kwa kutumia mtandao.

Nae Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USCAF)  Justina Mashiba amesema  mfuko wao utafadhili maabara ya TEHAMA katika shule ya Msingi ikiwa ni hatua ya kuwajengea msingi wa TEHAMA kuanzia wakiwa wadogo.

Akizungumzia maendeleo ya matayarisho ya kijiji cha Msomera kupokea wageni kutoka Ngorongoro Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe amesema Kijiji cha Msomero kiko tayari kupokea wageni  ambapo huduma zote za msingi ikiwepo makazi, maji, umeme, shule, majosho na maji kwa ajili ya mifugo yako tayari.

No comments:

Post a Comment

Pages