Dar es Salaam, Tanzania
Airtel Tanzania imekabididhi zawadi kwa washindi wawili wa droo kubwa ya promosheni ya TESA KIMILIONEA INAEDELEA, mshindi mmoja amekabidhiwa gari mpya aina ya Toyota RAV4 na wa pili pesa taslimu Tshs 10 milioni.
Washindi hao ni
John Mathayo, mkazi wa Bunju na mfanya biashara wa nyanya na Ibrahim
Dyamwala ambaye ni mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam.
Wateja na
Mawakala walikuwa na nafasi ya kuingia kwenye droo ya kwa kutumia moja
ya huduma za kuweka pesa, kutuma pesa Airtel kwenda Airtel, kutoa pesa,
kulipia bili kwa kutumia huduma ya Airtel Money ya promosheni ya TESA
ZAIDI KIMILIONEA na kujishindia Tshs 1 milioni kila siku au gari mpya
aina ya Toyota RAV4 na pesa taslimu Tshs 10 milioni kwenye droo kubwa.
Kwa
upande wake, mshindi wa zawadi ya Tshs 10 milioni Ibrahim Dyamwala
alisema ‘Nilikuwa siamini kama ni kweli Naweza kuwa nimeshinda hii
zawadi ya Tshs 10 milioni. Kwa leo nimeamini na nawashukuru Airtel kwani
kwa sasa nitaweza kukamilisha ujenzi wa nyumba yangu pamoja na kuongeza
uwekezaji kwenye kilimo. Naomba kuwahidi kuwa nitaendelea kutumia
bidhaa za Airtel pamoja na kuwahimiza ndugu, jamaa na marafiki juu ya
umuhimu wa kutumia Airtel Money.
No comments:
Post a Comment