HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2022

WAZIRI WA UWEKEZAJI DK. ASHATU KIJAJI ATEMBELEA BANDA LA UTT AMIS KATIKA MAONYESHO YA SABASABA 2022

 

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk, Ashatu Kijaji, akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko Mkuu wa UTT AMIS, Mfaume Kimario, kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango.

Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Kassim Msemo (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS, Rahim Mwanga (kushoto), alipofika kujionea huduma na elimu inayotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Dk. Nichalaus Shombe, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la UTT AMIS katika maonyesho ya Sabasaba.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya UTT AMIS, Daudi Mbaga, akitoa ufafanuzi kwa wateja waliofika katika Banda la kampuni hiyo katika viwanja vya Sabasaba. 
Afisa Masoko Mkuu wa UTT AMIS, Mfaume Kimario, akitoa maelezo kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya UTT AMIS.

Afisa Uendeshaji wa UTT AMIS, Nuru Chimwenda, akitoa ufafanuzi kwa wateja waliofika katika Banda la kampuni hiyo katika viwanja vya Sabasaba.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Doris Mlenge, akitoa maelezo kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya UTT AMIS. 
 Wananchi
wakipata maelezo kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya UTT AMIS.

 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya UTT AMIS, Daudi Mbaga (wa tatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa UTT AMIS ndani ya banda lao katika maonyesho ya Sabasaba Dar es Salaam.
 

No comments:

Post a Comment

Pages