HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2022

Nape atoa wito kwa wananchi kuendelea kutumia huduma zitolewazo na Shirika la Posta Tanzania


Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu TANTRADE, Latifa Khamis (kulia) Mkurugenzi mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga (kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa UCSAF Bi. Justina Mashiba (wa pili kushoto) wakisubiri kumpokea Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati wa hafla ya Siku ya Posta iliyofanyika katika viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Nape Nnauye, akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Posta iliyofanyika katika viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam. 

 

Na Mwandishi Wetu

 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Nape Nnauye, atoa wito kwa wananchi kuendelea kutumia huduma za Shirika la Posta kwani kwa sasa Shirika limeboresha huduma zake kuwa za kisasa kulingana na mahitaji ya wananchi.


Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam wakati alipohudhuria Siku maalum ya Shirika la Posta katika viwanja vya Maonesho ya 46 Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam

Aidha, Waziri ametumia nafasi hiyo kulipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa juhudi inayoendelea kuzifanya katika kutoa huduma bora na stahiki kulingana na mahitaji ya wananchi hususani katika kipindi hiki cha maendelea ya TEHAMA

Sambamba na hilo,  Nape amepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali viwanjani hapo ikiwemo Banda la Shirika la Posta Tanzania na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika viwanja hivyo 

Naye, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo ameelezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo viwanjani hapo ikiwemo huduma za EMS, Duka Mtandao, Posta Kiganjani, Huduma za kubadilisha fedha za kigeni na Uwakala ikiwemo ukataji wa tiketi za ndege ya ATCL

Pia, Postamasta Mkuu ametumia nafasi hiyo kuendelea kuwakaribisha wananchi katika banda la Posta lililopo viwanjani hapo ili kuendelea kufurahia huduma za kisasa

Hafla hiyo ya Siku maalum ya Posta imehudhuriwa Viongozi waandamizi na wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania pamoja na wasanii mbalimbali wa maigizo (Bongo Movie) ikiwemo Swebe, Snura, Tausi Mdegela, Dr Kumbuka, Asha Boko, na wengine mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages