Mkuu wa Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli (katikati), Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania , Mercy Silla (kulia) na Makamu Mwenyekiti, Rose Romanus (kushoto), wakifuarahi baada ya kuzindua Siku ya NMB iliyoadhimishwa na Chama Cha wafanyabiashara wanawake Tanzania kwenye maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya NMB imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwawezesha wanawake
wajasiriamali kote nchini ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuhakikisha
wanawake wanapiga hatua kiuchumi.
Benki
hiyo kati ya Julai 2021 hadi Juni 2022 ilitoa mikopo 37,501 kwa
Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SMEs) yenye thamani ya bilionin 752.7-
huku idadi kubwa ikilenga wafanyabiashara wadogo na wa kati wanawake kwa
mujibu wa Afisa Mkuu Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB Nenyuata
Mejooli.
Akizungumza
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya NMB, hafla iliyoandaliwa na benki hiyo
kwenye banda la Chama cha Wanawake Wafanyabiashara (TWCC) kwenye
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea
kwa ajili ya kuwakumbuka wanawake wajasiriamali, Mejooli alisema benki
yake imeweza kubuni bidha mbali mbali ikiwa ni mkakati mahususi wa
uwezeshaji wanawake na kuongeza kuwa tangu mwaka 2000, benki imekuwa
ikitoa mikopo midogo kuanzia shilingi laki 5 hadi milioni 75.
Alisema
kutokana na dhamira ya benki yake, NMB awali mwaka huu iliorodhesha
hati iliyopewa jina la NMB Jasiri Bond katika soko la hisa la Dar es
Salaam ambayo ilikusanya bilioni 74.2 ikilenga biashara zinazomilikiwa
na wanawake.
"Fedha
zilizopatikana zitatumika kusaidia biashara zinazomilikiwa na wanawake
au wafanyabiashara ambao mnyororo wao wa thamani unanufaisha wanawake
wengi. Natoa wito kwa wanawake wajasiriamali kuchangamkia fursa
tunapoanza kutoa mikopo,” alisema.
Aliongeza
kuwa benki yake tayari imetoa bilioni 95.1-katika miaka mitatu
iliyopita kama sehemu ya juhudi zake za kusaidia ukuaji wa biashara
zinazomilikiwa na wanawake kote nchini.
“Kama
benki, tunaelewa kuwa bado kuna idadi kubwa ya watu ambao hawapo kwenye
mfumo rasmi wa kifedha ndiyo maana tukaja na kampeni yetu ya malipo ya
kidijitali inayoitwa “Teleza Kidigitali inayolenga kuongeza
ushirikishwaji wa fedha kupitia bidhaa kama vile NMB MshikoFasta, NMB
Pesa Wakala na Lipa Mkononi. Tutaendelea kuwekeza katika utafiti ili
kubuni bidhaa nyingi zaidi za kifedha ili kupunguza gepu ya watu ambao
hawapo kwenye mfumo rasmi,” alisema.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mercy
Silla wakati wa hafla hiyo aliishukuru benki hiyo kwa kuendelea kusaidia
kuwawezesha wanawake wajasiriamali na kuongeza kuwa chama chake
kitaendelea kushirikiana na kusaidia wanawake katika ngazi za chini
Alibainisha
kuwa wanawake bado wana fursa nyingi hukuakibainisha kuwa asilimia 30
ya bajeti ya manunuzi imetengwa kwa ajili ya wanawake ikiwa ni sehemu ya
jitihada za kuimarisha ushiriki wa wanawake katika mchakato wa manunuzi
na kuwataka wanawake kushiriki kikamilifu katika mchakato wa zabuni na
kutumia fursa za manunuzi katika miradi mbalimbali.
"Kuna
fursa zimewekwa kwa wanawake katika mchakato wa zabuni na manunuzi
lakini kwa bahati mbaya wanawake hawajaweza kushiriki kikamilifu na
kunyakua fursa kama hizo. Wanawake wanahitaji kutumia fursa hizi zote
kikamilifu. Kama chama, tutaendelea kuhamasisha wanawake kuhusu jinsi ya
kunyakua fursa kama hizo kuanzia ngazi ya chini,” alisema.
Maadhimisho
ya Siku ya NMB yalifanyika chini ya kaulimbiu ya “Kuwawezesha Wanawake
katika Biashara” yamewakutanisha wanawake kutoka mikoa ya Dar es Salaam,
Simiyu, Tanga, Mara, Njombe, Mwanza kutoka sekta ya usindikaji wa
vyakula, nguo, ngozi, vipodozi, afya na kazi za mikono.
No comments:
Post a Comment