HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2022

Profesa arudisha mshahara wa Tsh mil. 58.7

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni hivi ndivyo unavyoweza kusema kwa Profesa Lallan Kumar ambaye ni Mhadhiri wa Chuo kiitwacho Nitishwar nchini India ameamua kurudisha mshahara wake wa miaka miwili kwa sababu wanafunzi hawajatokea darasani kuhudhuria somo analofundisha.

Vyombo vya habari nchini India viliripoti kuwa Lallan Kumar ambaye ni Profesa msaidizi wa lugha ya Kihindi katika chuo cha Nitishwar jimbo la kaskazini India la Bihar amerudisha kwa chuo hicho mshahara wenye thamani ya £uro 25,108 ambazo ni sawa na Tsh. milioni 58.7.

“Hakuna mwanafunzi aliyefika darasani ili kufundishwa sasa mshahara ni wa nini?” alisema Profesa Kumar.

NDTV India wameripoti kwamba Mkuu wa Chuo amesema madarasa yalitatizwa kutokana na janga la corona japo Profesa Kumar anasema kitendo cha Wanafunzi kutotokea kwenye madarasa yake kimemfanya aogope "kifo cha kitaaluma" kwenye kazi yake.

No comments:

Post a Comment

Pages