Dk. Mngerza Miraji (kushoto) aliyekua katibu Mkuu Wizara Maji, Nishati na Madini na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar akimkabidhi katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo, Joseph Kilangi, nyaraka za wizara hiyo baada kusaini fomu ya makabidhiano.
Na Talib Ussi, Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kupitia Wizara ya Maji, Nishati na Madini
imeingiza mapato ya shilingi bilioni tatu na milioni hamsini na sita
kwa kipindi cha miezi mitatu ikiwa ni mauzo ya maliasili zisizorejesheka
ikiwemo kifusi, mchanga mawe, kokoto na vumbi.
Hayo
yameelezwa na aliyekuwa katibu mkuu wa wizaya hiyo Dkt Mngerza Mzee
Miraji wakati akimkabidhi ofisi katibu mkuu mpya wa wizara hiyo Joseph John Kilangi aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya Ardhi na
Maendeleo ya Makaazi.
Dkt.
Mngereza amesema kutokana changamoto za upotevu wa maliasili kwa
kushirikiana na watendaji wake waliamua kuchukua hatua za makusudi
kuazisha mfumo wa kuombea maliasili zisizorejesheka ili kuzuia upotevu
mali hizo. Hivyo April hadi June wizara hiyo imeweza kuingiza fedha
hizo ambapo mwezi wa Juni pekee uliingiza shilingi bilioni moja na
nusu.
“Mfumo huu ni mzuri
sana kwani unaweza kuona gari inapoingia katika shimo la maliasili,
mali iliyobeba, uwezo wa gari, na wapi inaelekea hali ya kuwa nipo
ofisini hata usiku. Pia mtu akilipa malipo benki kupitia mfumo huu
unaonesha fedha zilizoingia aina zote za malipo kuanzi kibali shilingi
3000, kutokana na kamera zilizofungwa. Hii ndio ilikuwa kazi ngumu ya
kudhibiti upotevu wa maliasili” alisema Mngereza
Aidha
Dkt. Mgereza aliwashukuru watendaji kazi wa wizara hiyo kwa mashikiano
makubwa waliyompa katika kipindi chote alichotumika wizara hiyo kwani
walikuwa wakifanya kazi kwa mashikiano ya karibu hali ambayo imeonesha
dhamira ya Serikali katika kuwaletea wananchi wake maendelo.
Kwa
Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Joseph J. Kilangi aliyekabidhiwa
amesema anaamini yote aliyokabidhiwa atayaendeleza kwa dhati ile ile
hivyo, amewaomba watendaji wa wizara hiyo kumpa mashirikina kama
walivyompa Dkt Mngereza kwasababu wote wanajenga nyumba moja ya
kutekeleza ahadi za Serikali ya awamu ya nane inayongoza na Dkt Hussein
Mwinyi.
Aidha amewataka
watendaji wa wizara hiyo kutomchoka mapema kutokana na kuwaita mara kwa
mara kwani majukumu hayo ni mapya kwake hivyo anahitaji kujifunza mambo
mengi kupitia kwao. Amesema anaamini akipewa mashirikiano hakuna
kitakacho mshinda kwani kinachohitajika ni uwazi na uwajibikaji.
Mapema
Waziri wa wizara hiyo amemshukuru Dkt Mngereza kwa mashirikiano makubwa
aliyompa pamoja na juhudi za kuanzisha mfumo huo. Amesema mashirikinao
ya Dr Mngereza yameweza kufanikisha bajeti ya wizara hiyo kupita kwa
urahisi hivyo amewataka watendaji wa wizara hiyo, kuendeleza ili ufanisi
upatikane.
Makabidhiano
hayo yamekuja kufuatia uteuzi aliyoufanya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapiduzi Zanzibar Dkt Hussein siku ya June 30,2022 wa
kuwateua manaibu katibu mkuu pamoja kuwabadilisha makatibu wakuu wa
wizara mbali mbali za SMZ.
No comments:
Post a Comment