HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 01, 2022

WAZIRI AWESO AZINDUA BODI YA NNE YA MAJI YA TAIFA


Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akikata utepe akikata utepe wakati akizindua Bodi ya Nne ya Maji ya Taifa. 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa wana kazi kubwa ya kuishirikisha jamii  kulinda rasilimali za maji kwani maji hayo ndio moyo  katika mageuzi ya kiuchumi.


Haya ameyasema Juni 30,2022 jijini hapa  wakati akizindua Bodi ya Maji ya Taifa Waziri huyo amesema kuwa suala la kutunza rasilimali za maji ni jukumu la watu wote.


Amesema kuwa sasa wanajivunia mafanikio makubwa ya ikiwemo kwa mara ya kwanza bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa kwa asilimia 100.


Waziri Aweso ameongeza ilikuwa  ni aibu na fedheha kuwa  Wizara ya lawama  ambapo kwa sasa wana mengi ya kujivunia kwani hata ile miradi chechefu wamefanikiwa kukwamua miradi 126.


" Tuipa nguvu kubwa rasilimali za maji ambazo ndio moyo katika kuleta mageuzi ya kiuchumi  sasa ni muda muafaka wa kuwa na mpango Mkuu wa raslimali za maji," amesema.


Waziri Aweso ameeleza kuwa bodi za maji za mabonde kufanya udhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji na mchakato wa sheria uko mbioni kukamilika.


Alisema kuwa mipango ya matumizi ya maji ni muhimu katika uluaji wa uchumi Ili kuwa na raslimali za maji endelevu.


Waziri Aweso amitaka Bodi iliyoingia madarakami kufanya kazi zake kwa weledi huku akisema ushauri uliptolewa na bodi ya tatu wataufanyia kazi ili kuhakikisha rasilimali za maji zinaleta manufaa kwa Watanzania.


Naibu Waziri wa Maji MaryPrisca Mahindi amesema kuwa lengo kubwa ni kuumtua mama ndoo kichwani huku akiitaka  Bodi hiyo  ya nne kuvaa viatu vilivyovaliwa na bodi ya tatu lengo kubwa ni kuona Wizara inasonga mbele zaidi .


Katibu Mkuu Wizara ya Maji  Mhandisi Antony Sanga amefafanua  kuwa misingi ya yote wanaoifanya ni kuwapatia wananchi maji bora na salama.


" Tumepiga hatua kubwa kutoka  Wizara ya lawama hadi kuwa  Wizara ya utatuzi.Maboresho ni makubwa sana yaliyofanyika haya ni mapinduzi makubwa  ya kujivunia" amesema.


Mkurugenzi wa Rasilimali za maji kutoka Wizara ya Maji, Dk George Lugomela alisema kuwa Bodi hiyo iliteuliwa rasmi Aprili 2021 na Bodi inaundwa  na Mwenyekiti na wajumbe 11.


Amesema kuwa kazi kuu wa bodi hiyo ni kumshauri Waziri juu ya masuala yanayohusu raslimali za maji na utatuzi wa migogoro wenye sura ya Kitaifa na kimataifa.


"Bodi hii pamoja na jukumu la kumshauri Waziri ipewe meno ya kudhibiti shughuli za mabonde ya maji , ipewe meno kidogo isiwe ya kushauri tu," alisema.


Mwenyekiti wa Bodi ya nne' ya Taifa ya maji Mhandisi Mbogo Mfutakamba amesema watatekeleza majukumu yao kwa weledi.

No comments:

Post a Comment

Pages