b1:
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndg Abdulrahman
Kinana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Abubakar Zubeir bi
Ali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muliro
(kushoto) na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa
Taasisi ya Mohamed VI Foundation Dkt. Sidi Mohamed Rifki mara baada ya
ufunguzi wa Mashindano makubwa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu
yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mfalme Mohamed VI (Mohamed VI Foundation)
katika Masikiti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)
Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Agosti 12, 2022.
b2:
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwa katika
picha ya kumbukumbu na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt.
Abubakar Zubeir bi Ali, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mohamed VI Foundation
Dkt. Sidi Mohamed Rifki (wa tatu toka kulia) pamoja na viongozi wengine
mara baada ya ufunguzi wa Mashindano makubwa ya kusoma na kuhifadhi
Quran Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mfalme Mohamed VI (Mohamed VI
Foundation) katika Masikiti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Agosti 12,
2022. Picha na Issa Michuzi.
Na Issa Michuzi, Kinondoni
Mashindano
makubwa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi
ya Mfalme Mohamed VI (Mohamed VI Foundation) wa Morocco yamefunguliwa
rasmi leo katika Masikiti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam huku nchi 35
zikishiriki.
Pamoja
na mashindano hayo, ambayo ni katika awamu yake ya tatu yakiwa
yameanzia nchini Morocco na kisha Senegal, pia kuna maonesho maalum ya
Quran ikiwa ni pamoja na jinsi kitabu hicho Kitukufu kwa Waislamu
duniani kinavyoandikwa kwa mkono na kwa mashine.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi alihudhuria ufunguzi
huo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Bara, Ndg Abdulrahman Kinana, aliyewaongoza maelfu ya waumini
katika hafla hiyo iliyoambatana na Swala ya Ijumaa.
Ndg
Kinana amemshukuru Mfalme wa Morocco sio tu kwa kuichagua Tanzania kuwa
nchi ya tatu kuandaa mashindano hayo makubwa bali pia kwa kujenga
msikiti huo mkubwa kuliko yote katika nchi za Afrika Mashariki na kati,
kufuatia ziara yake nchini mnamo Oktoba 2016.
"Ziara
hiyo ya Mfalme Mohamed VI nchini imeendeleza uhusiano mwema uliopo kati
ya nchi hizi mbili pamoja na kufungua milango ya nyanja mbalimbali
ikiwemo dini na bishara", amesema Ndg. Kinana.
Katibu
Mkuu wa Taasisi ya Mohamed VI Foundation Dkt Sidi Mohamed Rifki
ameusifia uongozi wa tawi la Taasisi hiyo nchini chini ya Mwenyekiti
wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Abubakar Zubeir bi Ali,
kwa weledi mkubwa uliotumika katika kuandaa mashindano hayo.
Dkt.
Rifki amelihakikishia Tawi la Taasisi hiyo nchini utekelezaji wa
programu zake kwa mujibu wa maazimio iliyoijiwekea ya kuendeleza dini na
vijana, pamoja na kuendeleza umoja wa wana Ulamaa katika kuhakikisha
usalama, Uimara na maendeleo ya bara la Afrika.
Mufti
na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Abubakar Zubeir bi Ali amewataka
Watanzania bila kujali itikadi ya dini kuhudhuria mashindano hayo ambayo
yanafikia tamati siku ya Jumapili.
No comments:
Post a Comment