Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Peter Serukamba (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022, Sahili Nyanzabara Geraruma na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MWENGE wa Uhuru umepokelewa leo (Agosti 9, 2022) mkoani Singida ukitokea
mkoa wa Tabora ambapo ukiiwa Singida utazindua na kuweka jiwe la msingi kwenye
miradi yenye thamani ya shilingi 8,280,426,339.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akitoa taarifa ya mkoa wakati wa
kupokea Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Mseko wilayani Iramba, alisema katika
utekelezaji wa miradi hiyo nguvu za wananchi ni Sh.84,203,100,, halmashauri
shilingi 173,296,344, Serikali Kuu shilingi 6,449,362,831 na wahisani shilingi 1,575,742,564.
Ifuatayo ni baadhi ya mambo aliyoyaongea Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.
Serukamba katika risala yake :-
PONGEZI KWA RAIS SAMIA SULUHU
HASSANI
Serikali ya Mkoa wa Singida na wananchi wote tunatoa pongezi kwa Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa moyo na upendo
mkubwa kwa Watanzania hasa katika uboreshaji huduma za afya, barabara, elimu na
maji.
Katika kipindi cha uongozi Awamu ya Sita Mkoa wa Singida umepokea jumla ya
shilingi 270,371,690,554.00 kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Wadau
mbalimbali wa kwenye miradi ya Maendeleo katika sekta Elimu, Afya, Utawala,
Kilimo, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Sekta Ya Barabara, Nishati, Maji, Habari
Na Mawasiliano.
Katika sekta ya Elimu jumla ya shilingi 30,571,875,316.74 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya Elimu pamoja na utoaji wa
Elimu Bila Malipo.
Jumla ya madarasa 236 yamepatiwa fedha za ukamilishaji na madarasa mapya
801 yamejengwa, jumla ya matundu ya vyoo 827 yamejengwa, jumla ya maabara 83
zimekamilishwa na ujenzi wa mabweni 4,.
Sekta ya Afya jumla ya shilingi 28,407,068,716.19 kwa ajili ya ujenzi wa
hospitali 4, vituo vya afya 15 na ujenzi wa zahanati utoaji wa chanjo na ujenzi
wa vyoo katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Katika eneo la Utawala jumla ya shilingi 5,090,191,781.28 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 23 za watumishi
na ujenzi wa majengo 3 ya Ofisi.
Katika Sekta ya Kilimo jumla ya tani 486.773 za mbegu za alizeti zenye
ruzuku ya Serikali ya thamani ya shilingi 2,260,755,000.00 zilitolewa kwa
wakulima wa Mkoa wa Singida zilitolewa.
Kwenye eneo la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi jumla ya shilingi
12,076,417,785.08 zilitolewa kupitia TASAF III kwa kaya maskini na fedha
zilizokopeshwa kwa vikundi 409 vya wanawake na vijana na watu wenye ulemavu.
Sekta ya Nishati imewezeshwa kutekeleza miradi yenye thamani ya shilingi
63,507,622,522.00 ya umeme ili kukamilisha vijiji 176 vya Mkoa wa Singida
ambavyo havijafikiwa na umeme.
Sekta ya Barabara jumla ya miradi yenye thamni ya shilingi
97,690,067,211.00 imetekelezwa na mingine inaendelea kutekelezwa kujenga
madaraja, matengenezo madogo na ujenzi wa barabara kaatika Mkoa wetu, vilevile
Mkoa kupitia sekta ya Habari na Mawasiliano ulipatiwa shilingi 816,292,481.00
kuweka anwani za makazi .
Uongozi wa Mkoa na wananchi wote wa
Singida tunamuunga Mkono Rais kwa kufanya kazi kwa bidii, kuthamini rasilimali
zetu na kuzitumia kwa uaminifu mkubwa ili kuleta maendeleo yenye tija kwa Taifa
letu. Tunaomba Mwenyezi Mungu ampe afya
njema ili kazi iendelee!
SENSA YA WATU NA MAKAZI
Mwaka huu Taifa letu litatekeleza zoezi muhimu la Sensa ya Watu na Makazi,
Mkoa wa Singida umejipanga kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa.
Maandalizi ya Sensa 2022 yamefanyika ambayo yanajumuisha Utengaji wa maeneo
2,501 yametengwa kama ifuatavyo; Singida Mjini (295), Manyoni (279), Itigi
(173), Ikungi (539), Singida Vijijini (434), Mkalama (388) na Iramba (393).
Uundaji wa Kamati za Sensa, Sensa ya Majaribio, Ajira za Makarani, kufanya
mafunzo ngazi ya Mkoa na Mafunzo kwa wasimamizi ngazi ya II (Mkoa) yamekwisha
fanyika.
Aidha mafunzo ngazi ya III ambayo
yalianza rasmi tarehe 31 Julai 2022 hadi 19 Agosti 2022 kufundisha wasimamizi
na makarani wa Sensa .
Moja ya maandalizi ya Sensa ni pamoja na kukamilisha ajira za muda za
Makarani na Wasimamizi wa Sensa na kuanza mafunzo tarehe 31 Julai 2022 ngazi ya
Wilaya.
Jumla ya makarani na wasimamizi wa Sensa wapatao 5,449 wameajiriwa
katika Mkoa ikiwa ni kipaumbale kwa vijana wasio na ajira.
Ili kufanikisha zoezi la Sensa, Kamati za Sensa katika ngazi zote za
kiutawala zimeundwa na zimefanya kazi ya elimu ya Sensa na kugawa vipeperushi
maeneo mbalimbali.
Mkoa umepokea takribani vipeperushi 30,000 ambavyo vilisambazwa kwenye
Halmashauri zote ili kuwafikia wananchi,uhamasihaji wa ushiriki wa wananchi
katika Sensa unaendelea kufanyika kupitia mikutano ya hadhara,vyombo vya
habari,mitandao ya kijamii pamoja na makongamano.
MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
Ili kuhakikisha tunatokomeza na kumaliza kabisa mizizi ya Rushwa, Mkoa wa
Singida unatambua na kupokea ujumbe mwambatano wa:-Mapambano dhidi ya Rushwa,
chini ya kauli mbiu, “KUZUIA RUSHWA NI JUKUMU LANGU”.
TAKUKURU Mkoa wa Singida Kipindi cha Mwezi Julai, 2021 hadi Julai, 2022
ilipokea taarifa 238 za vitendo vya rushwa kati ya hizo taarifa 61 zinaendelea
na uchunguzi na 22 zilifunguliwa kesi katika mahakama mbalimbali za Mkoa wa
Singida.
Aidha,Miradi ya maendeleo ilikaguliwa,elimu ilitolewa kwa wananchi kuhusu madhara ya rushwa kupitia
mikutano, Semina , maonesho, vipindi vya Redio
vimefanyika kupitia Standard Redio FM na kuimarishwa Klabu za wapinga
rushwa katika Shule za Msingi na
Sekondari.
HUDUMA ZA AFYA
Mkoa unaendelea na Mapambano dhidi ya Malaria, chini ya kauli mbiu “Ziro
Malaria Inaanza na Mimi nachukua hatua kuitokomeza”.
Kiwango cha Maambukizi ya Malaria Mkoa wa Singida ni 2.3%, ukilinganisha na
wastani wa kitaifa wa asilimia 7.3 wa maambukizi ya malaria.
Mkoa umelenga kuimarisha maeneo yafuatayo: Kinga, Upimaji na tiba,
Ushirikiano na Wadau wa Afya pamoja na kuimarisha mikakati mtambuka.
Eneo la Kinga: Mkoa kwa kushirikiana na OR - TAMISEMI na Mpango wa Taifa wa
Kudhibiti Malaria (NMCP) inatekeleza mpango wa kugawa vyandarua vyenye
viuatilifu kupitia shule za msingi za Serikali na Binafsi kwenye Halmashauri
sita (6) za Ikungi, Iramba, Itigi, Manyoni, Mkalama na Singida.
Kiasi cha vyandarua 359,757
vinatarajia kugawiwa kwa wanafunzi wote wa shule za Msingi katika kipindi cha
Julai hadi Septemba 2022. Aidha, Kwa kipindi cha Januari hadi Juni, 2022
vyandarua vyenye viuatilifu 32,796 (95%) Viligawiwa kwa wajawazito na vyandarua
26,367 (95%) kwa watoto umri chini ya mwaka 1.
Mkoa unaendele kutoa huduma ya
chandarua Kliniki kupitia kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya, kutoa elimu
kwa kutumia mabango ya kudumu, vyombo vya habari, vituo vya kutolea huduma za
Afya na mikusanyiko.
Kutumia fursa zozote za uhamasishaji kuongeza mwitikio wa wananchi
kupambana na Malaria kwa kuonyesha matumizi endelevu ya vyandarua.
Eneo la Upimaji na Tiba: Mkoa unaendelea
kuimarisha upatikanaji wa dawa Mseto (ALu) na vipimo vya malaria (mRDT)
na upimaji wa Malaria kupitia hadubini.
Aidha, upimaji wa Malaria kupitia mRDT na matibabu kwa dawa za malaria (ALu
na Sindano ya Artesunate) zinatolewa
bila malipo katika Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya vya Serikali.
Kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2022 jumla ya wagonjwa wateja 137,299
walipimwa malaria ambapo kati yao 10,645 Waligundulika kuwa na vimelea vya
malaria na walipatiwa matibabu.
Ushirikiano na Wadau wa Afya: Mkoa unaendelea kushirikisha Viongozi wa dini, Viongozi wa
kisiasa, Sekta binafsi kutekeleza Afua mbalimbali zinazo lenga kupambana na
Malaria.
Mikakati Mtambuka: Mkoa unaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya ili kukabiliana na gharama za matibabu.
MAPAMBANO YA DAWA YA KULEVYA
Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, chini ya kauli mbiu; “Tuelimishane juu
ya Tatizo la Dawa za Kulevya, Kuokoa Maisha”.
Mkoa umejipanga kuendelea kutoa
elimu kuhusu madawa ya kulevya na athari zake kwa jamii kupitia shule, vikao,
mikutano, maadhimisho mbalimbali yanayofanyika ngazi za Halmashauri, Mkoa na
vyombo vya habari vilivyopo ndani ya Mkoa.
Vituo vya kutolea huduma za Afya vinatoa huduma kwa waathirika wa madawa ya
kulevya ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya athari za madawa ya kulevya, huduma
ya ushauri pamoja na dawa.
Waathirika wa madawa ya kulevya wengi wameathiriwa na bangi, kokaine,
ugoro, mirungi na pombe. Kwa kipindi cha mwaka 2021/22 jumla ya wagonjwa 80
wamehudumiwa na kupatiwa matibabu katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
No comments:
Post a Comment