Mradi wa wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ujulikanao Samia Housing Scheme (SHS) wa nyumba 5000 pekee unatarajiwa kutoa ajira zipatazo 26,400(direct 17,600 na indirect 8,800).
Taarifa hiyo imetolewa na Meneja Habari na Uhusiano wa NHC, Muungano Saguya alipokuwa akielezea mbele ya vyombo vya habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dodoma Agosti 8,2022 kuhusu utekelezaji wa shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na Mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Amesema utakuza mapato ya serikali mfano mradi wa SHS 5000 unatarajiwa kutengeneza mapato ya kodi mbalimbali za serikali TZS bilioni 50 (mauzo ya nyumba) bilioni 10( ununuzi vifaa vya ujenzi), PAYE TZS 17.8 bilion, Kodi ya majengo TZS milioni 55, corporate Tax kutoka NHC na wajenzi wengine bilioni 77, VAT 60bilioni.
Aidha, itakuza sekta ya fedha kupitia mikopo ya nyumba watengenezaji, wauzaji na wakondarasi watakopa asilimia hadi 60 ambayo ni sawa na TZS 194.8 bilioni.
Baadhi ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo.
PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment