Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
Na Victor Masangu, Pwani
Jeshi
la polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata
watu wapatao 21 kwa tuhuma za makosa mbali mbali likiwemo na kunasa
mtandao wa matapeli sugu wa mtandao wa matukio ya wizi wa mifugo pamoja
na utapeli wa ardhi.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani Pius
Lutumo amebainisha kuwa mtumumiwa mmoja wa wizi wa ng'ombe alipigwa
risasi na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali kwa ajili ya
matibabu.
Aidha Kamanda
alibainisha kuwa mtu mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa aliibjwa
ng'ombe wake nane baada ya kuvunjiwa zizi na watu ambao hawajulikani
ambapo walinzi wawili wachungaji waliokuwa wakilinda katika kambi hiyo
walikamatwa na wahalifu.
Alifafanua
kuwa katika tukio hilo mchungaji mmoja alifanikiwa kuwatoroka wahalifu
hao baada ya kujeruhiwa mkonini huku mwenzake aliyejulikana kwa jina la
Ally Msonde alipoteza maisha yake baada kukutwa porini akiwa amekatwa
shingoni na kitu chenye ncha kali shingoni.
Katika
hatua nyingine Jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa
majina ya Mariam Patrick kwa tuhuma za kumtapeli kiasi cha shilingi
zaidi ya milioni tisa askofu wa kanisa la mlima wa mabadiliko aitwaye
Modestus Ndago.
Aidha
Jeshi la Polisi limemtaka mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Hassan
Kanyuanyua kujisalimisha mara moja katika kituo Cha polisi kwa tuhuma za
kufanya utapeli wa viwanja.
Kadhalika
Jeshi hilo limetoa wito kwa mtu yoyote ambaye anajihusisha na mtandao
wa uuzaji wa viwanja na mashamba pasipo njia ya halali kuachana na tabia
hiyo mara moja kwani kunasababisha kuibuka kwa migogoro ya ardhi.
No comments:
Post a Comment