HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 26, 2022

SERIKALI YATOA PIKIPIKI KWA RUWASA, JUMUIYA ZA WATUMIA MAJI SINGIDA


Mkuu wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba (katikati) akikata utepe kuashiria kuzipokea na kuzigawa pikipiki tisa kwa Jumuiya za Watumia Maji (CBWSOs) na kwa watendaji wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika hafla iliyofanyika leo Agosti 22,2022 katika Ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Kati mjini hapa. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidi anayeshughulikia Uzalishaji na Uchumi Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida, Lucas Said na Afisa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati, Danford Samson.

 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amewagiza wataalam wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)  kuhakikisha miradi yote ambayo serikali inaingia mikataba na wakandarasi inasimamiwa vizuri ili iweze kumalizika kwa wakati na kujengwa kwa ufanisi.

Ametoa agizo hilo jana wakati akikabidhi pikipiki tisa kwa watumishi wa RUWASA wa wilaya za Singida,Ikungi,Manyoni,Mkalama, Mamlaka ya Maji Kiomboi,Jumuiya za Watumia Maji (CBWSOs) za Ikungi, Iramba na Manyoni .

Pikipiki hizo zenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 29.2 zimetolewa na Wizara ya Maji kwa lengo la kuwarahisishia utendaji kazi.

"Wataalam muendelee na usimamizi wa miradi ya maji kwa weledi kuhakikisha miradi yote tunayoingia mikataba na wakandarasi au inayojengwa kwa utaratibu wa 'force account' inasimamiwa vizuri na inajengwa kwa mujibu wa 'specification' na 'standards' zilizowekwa," alisema.

Serukamba alisema wataalam wahakikishe  pikipiki hizo zinatumika kwa shughuli za usimamizi na uendeshaju wa miradi ya maji katika ngazi zote za wilaya na jumuiya na zitunzwe ili ziweze kutumika kwa muda mrefu.

Mkuu wa Mkoa aliwataka watendaji wa RUWASA kuzingatia bei elekezi za mauzo ya maji vijijini ambazo zimekuwa kero kwa wananchi wa vijijini kwa kila Jumuiya ya Watumiaji Maji ipange bei ya maji kwa kuzingatia teknolojia inayotumika kusukuma maji.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida, Lucas Said, alisema hali ya upatikanaji wa maji vijijini kwa mkoa huu unakadiriwa kufikia asilimia 61.40 hadi kufikia Juni 2022.

Alisema katika utekelezaji wa bajeti ya 2021/2022 kupitia RUWASA Singida ilidhinishiwa Sh.Bilionj 14.9 zikiwa ni fedha za maendeleo ambapo hadi kufikia Juni 2022 fedha zikizokuwa zimepokelewa ni Sh.bilioni 14.7sawa na zaidi ya asilimia 97 ya bajeti.

Alisema fedha hizo zimetumika kutekeleza miradi 47 ya maji katika halmashauri sits za Mkoa wa Singida na kwamba katika mwaka huu wa bajeti wa 2022/2023 mkoa umetengewa Sh.bilioni 13.4 ambazo zitajenga miradi 42.

"RUWASA Mkoa wa Singida ina jumla ya vyombo 134 vya utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSOs) ambapo katika kuhakikisha huduma za maji inapatikana vijijini RUWASA makao makuu imeendelea kuwezesha ofisi za RUWASA ngazi ya wikaya, Mamlaka ya Maji Kiomboi na Vyombo vya Utoa Huduma Ngazi ya Jamii," alisema.


No comments:

Post a Comment

Pages